1 |
Anasema hatua hiyo ina mchango mkubwa katika kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati. Anatoa mwito kwa Watanzania hasa wale wa kipato cha chini kuendelea kujiunga na benki yake ili waweze kupata huduma bora kwa gharama nafuu, huduma ambazo anasema zitasaidia kukuza kipato chao. |
2 |
Alimshukuru Mkurugenzi wa Matomondo One, Daniel Msembele kwa kujitoa na kuanzisha miradi hiyo itakayoongeza ajira kwa wananchi wa maeneo hayo na kuinua uhitaji wa malighafi inayotoka kwa wakulima, na itachochea ukuaji wa soko kati ya mataifa ya Msumbiji na Tanzania kwa kuwa wapo karibu na mpaka. |
3 |
Mtaka alisema kwa Kanda ya Ziwa hakuna mkoa wenye uoto wa asili na wenye kuvutia wawekezaji kama mkoa wa simiyu, hivyo sasa hii ni fursa kwa watu kama Benki ya Maendeleo ya Kilimo walivyoiona na kuja kutaka kuwekeza mkoa humu kuweza kuja kujenga viwanda na kutoa ajira kwa watu wake. |
4 |
Viashiria vingine ni shughuli za kilimo, makazi ya kaya na upatikanaji wa maji, matumizi na usalama wa chakula katika kaya, maamuzi katika kaya, ukatili kwa wanawake na matarajio ya vijana, mahusiano ya kaya na jamii pamoja na mtazamo wa kaya kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. |
5 |
Aliitaja kuwa ni kugharamia elimumsingi bila malipo, kupanua ruzuku na mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ununuzi wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, ukarabatri na upanuzi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma na ujenzi wa vyuo vitano katika mikoa ya Geita, Simiyu, Njombe, Rukwa na Kagera. |
6 |
Balozi Amina alikiri na kusema ni kweli bidhaa zinazozalishwa Zanzibar zimezuiliwa kuingia Tanzania Bara, wakati zile zinazozalishwa bara zipo kwa wingi katika soko la Zanzibar. Alisema tatizo hilo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na ngazi za watendaji na sio sera ya biashara ya taifa inavyoelekeza. |
7 |
Ofisa Mikopo wa Benki ya Akiba mkoani hapa, Stephen Mtakati alisema hayo jana wakati wa mahojiano kwenye maonesho ya mifuko ya uwezeshaji na taasisi mbalimbali yanayoendelea katika viwanja vya mashujaa Mjini hapa. Alisema Benki hiyo iko kwenye mikakati ya kuanzisha mradi wa kunenepusha ng'ombe. |
8 |
Aidha amesema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi na kwamba kwa kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia. Amesema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi. |
9 |
Tuna kila sababu ya kumtakia kila la heri Rais Kenyatta na Naibu Rais, Ruto, kwa kuwa wameonesha ukomavu wa kisiasa, ushapavu, uvumilivu na ustahimilivu wa hali ya juu hasa kutokana na kutangazwa washindi mara mbili, kufuatia kesi zilizokuwa zinafunguliwa na vyama vya upinzani. |
10 |
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, uchaguzi unaomweka Kenyatta madarakni leo, ulikuwa huru na wa haki, unaoaminika na wenye mafanikio kwenye mazingira magumu huku ikisisitiza kwamba Kenyatta atazingatia suala la amani, mafanikio, matakwa ya Katiba na mapatano. |
11 |
Tunaziomba nchi nyingine za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika, majirani na hata jumuiya za kimataifa, kuiunga mkono Serikali mpya itakayoingia madarakani hivi karibuni. Hata hivyo, tunaamini yaliyotokea Zimbabwe yatabaki kuwa somo kwa wanasiasa mbalimbali na hata wananchi katika utekelezaji demokrasia. |
12 |
Huko nyuma tuliona wachezaji wetu baadhi yao walikuwa wakishangaa hata viwanja vya wenzetu jinsi vilivyo vikubwa na vizuri, lakini kwa sasa hilo halipo tena, kwani hata sisi tuna uwanja unaofanana na vile vya Ulaya kwa ubora wa sehemu ya kuchezea na mahali pa kukaa watazamaji. |
13 |
Muhimu ni kuiandaa vizuri timu yetu kwa ajili ya kucheza na timu zenye uwezo zaidi yetu ili tuweze kuambulia kitu fulani na siyo kucheza na timu zilizopo chini yetu. Mchezo dhidi ya Benin angalau tulicheza na wenzetu waliopo juu yetu, hivyo hapo tunaweza kupanda kidogo licha ya kutoka sare. |
14 |
Kwa mujibu wa Jafo, kitendo cha askari kuongoza magari katika barabara za mfumo huo, kinasababisha magari hayo kutofika vituoni kwa wakati. Jafo anasisitiza kuwa ni vema taa za kuongozea magari barabarani, zitumike ili mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka uweze kukidhi malengo yaliyokusudiwa. |
15 |
Wananchi wamekuwa wakidai kuwa kuchelewa kwa mabasi hayo vituoni, kunatokana na mfumo wa magari hayo kuingiliwa na trafiki, wanaoongoza magari katika taa. Ikumbukwe kuwa wananchi wanategemea mno mradi huo, ambao umekuwa mkombozi kwao, hivyo haitakiwi wakae vituoni muda mrefu kusubiri mabasi. |
16 |
Kuwafanya wananchi wasubiri vituoni muda mrefu, kuna athari mbalimbali kiuchumi na kijamii. Kiuchumi, wanachelewa kwenda kuzalisha mali na kuongeza kipato katika maeneo yao. Hali kadhalika, kuwachelewesha watu vituoni na kuwafanya walundikane, kiusalama siyo jambo zuri. |
17 |
Tunapenda kwanza kuchukua fursa hii kuzipongeza nchi za Tanzania na Liberia, kwa kujenga na kuuendeleza kwa makusudi utamaduni wa kidemokrasia wa kuachia madaraka ya juu ya nchi kupitia uchaguzi na hatimaye anayechaguliwa na wananchi, ndiye anayekabidhiwa kijiti cha uongozi. |
18 |
Hatuna shaka kwamba makubaliano ya kimataifa kuhusu kutoingilia masuala ya nchi nyingine, ni sheria tosha ya kimataifa na inayofaa kuzingatiwa si tu na taifa na serikali za nchi mbalimbali bali pia na kila mmoja kama tutataka maisha katika jamii yetu kuwa sawasawa na yenye kuwa na maana. |
19 |
Kwa kuwa wanaopitisha itifaki hizi ni wanasiasa na kwa kuwa wanasiasa ndiyo wanaovunja pia makubaliano tunawasihi wanasiasa nchini Tanzania kuwaacha Wakenya katika siasa zao za ndani bila wao kutia mkono kwa sababu mbalimbali ili mtangamano wa Afrika Mashariki uwe na maana ya kweli katika siasa. |
20 |
Hata kama tutakuwa tunajaribu kujitetea katika hili, lakini kitendo cha kuingilia kati siasa za Kenya kunakofanywa na wanasiasa wa Tanzania wengine wakiwa wameshawahi kuwa watawala nchini ni kuleta wingu zito linaloweza kuvunja matumaini na amani ambayo tayari ipo kwa Afrika mashariki. |
21 |
Hapa tungependa kuwakumbusha wenye dhamana katika sekta ya elimu katika ngazi ya kata, wilaya na mkoa, kufanya tathmini ya mahitaji hayo kupata kiwango kilichofikiwa na kampeni hiyo kitaifa katika kila shule ili kubaini uhaba uliopo na kuendeleza juhudi za kukabiliana nayo kwa vitendo. |
22 |
Kama serikali imechuka hatua za makusudi kuondoa ada, kwa nini kwa upande wa wazazi na walezi, wasichukue hatua za kukabiliana kwa vitendo tatizo la ukosefu wa madawati na viti kwa kuchangia kuokoa watoto wetu katika kadhia kama hiyo. Hili linawezekana, tuamke kukabiliana nalo. |
23 |
Kwa upande wa trafiki, wao wanalaumiwa kwa kusababisha foleni kwenye taa za Tazara, Keko na Ubungo. Wananchi wanadai kuwa trafiki wanaruhusu magari kwa upendeleo, hivyo mara nyingi kusababisha foleni. Jambo lingine kuhusu trafiki ni kushindwa kuingia ndani ya daladala na kukagua uozo uliopo. |
24 |
Wazo la ujenzi wa ofisi za walimu katika shule zetu ili walimu wafanyie kazi katika mazingira mazuri ni muhimu kwa manufaa ya watoto wetu na hatimaye taifa zima. Kwa msingi huo, ubunifu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, hauna budi kuigwa na kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote nchini. |
25 |
Kwa tukio hili, uongozi wa idara ya elimu pamoja na uongozi wa shule na serikali, uhakikishe unalifanyia uchunguzi suala hilo pia ili wafadhili waliojitolea kwa jambo hili muhimu kwa miundombinu ya shule, wasikatishwe tamaa kwa mbinu chafu za watu wachache kujinufaisha kutokana mchango huo. |
26 |
Hakuna ubishi kwamba kama hali hiyo haitatafutiwa suluhisho la kudumu, watoto wengi wa kike katika wilaya hiyo wataendelea kukatishwa tamaa katika harakati za kutimiza ndoto zao za kuwafikisha katika elimu ya juu na kupata ujuzi wa kuwasaidia maishani mwao, kama ilivyo wenzao wa kume. |
27 |
Tatizo la ukosefu wa hosteli au mabweni ya wasichana, halipo katika jimbo la Busega peke yake, bali pia majimbo na mikoa mingine hapa nchini. Hali kama hiyo ya wasichana kuingia katika vishawishi vya ngono na hatimaye kuishia kupata ujauzito, lipo pia katika maeneo hayo mengine. |
28 |
Tunawapongeza viongozi hao kwa kubuni tamasha hilo kuchangia shughuli za Ukimwi na pia kuwahusisha wanamichezo. Timu za Yanga, Simba, Mbeya City na Tanzania Prisons ni sehemu ya jamii ya wanamichezo na Watanzania hivyo zina wajibu wa kuchangia harambee hiyo kwa wachezaji wake kuonesha vipaji vyao. |
29 |
Hapa tungependa kuwakumbusha Watanzania kwa ujumla wake kwamba yeyote anayelenga kuwatenganisha Watanazania kwa kutumia mbinu yoyote ile, ikiwa ni pamoja na uchochezi ili kuharibu utamaduni wetu, tulioujenga kwa muda mrefu wa kuishi kwa amani na utulivu asipewe nafasi asilani katika taifa letu. |
30 |
Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika, ambazo zimekuwa zikipiga vita kwa vitendo ubaguzi wa aina yoyote ile ndani ya jamii, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa rangi, ukabila, dini na itikadi na badala yake kuhimiza ushirikiano na mshikamano katika nyanja za kujiletea maendeleo endelevu. |
31 |
Malori mamia kwa mamia yamekuwa yakisomba mchanga maeneo mengi ambayo hayajalengwa kwa biashara hiyo na vijana wamekuwa wakichimba hata maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za kijamii. Wakati mwingine wanavamia mashamba ya watu kwa vitisho wakitishia maisha ya wahusika. |
32 |
Pia tumuombe isiishie katika Mto wa Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko, bali baada ya muda atembelee na maeneo mengine aone uharibifu huu wa mazingira kutokana na wachimbaji kuharibu uoto wa asili kiholela na kuona kama agizo alilotoa juzi limetekelezwa na wahusika wanachukuliwa hatua. |
33 |
Tunaomba taasisi na makampuni mengine yaige kilichofanywa na Sport Pesa kuleta maendeleo katika maeneo ya kisekta. Tunaipongeza Sport Pesa kwa kuguswa na eneo la utalii na soka na kutumia fursa hii kuionesha dunia, mambo mazuri yaliyo nchini mwetu katika kuvuta watalii zaidi. |
34 |
Kwa makampuni mengine, hii ni fursa ambayo imewafumbua macho jinsi gani Serikali ilivyo tayari kushirikiana nao. Haitoshi tu kwa makampuni kutangaza wametumia mamilioni ya fedha kama huduma kwa jamii wakati kiasi hicho hakiakisi mapato yao na thamani ya rasilimali walizokabidhiwa kuvuna. |
35 |
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, juzi ilitangaza kutoa vibali kwa ajira hizo kujazwa. Tunapenda kuipongeza serikali kwa kuligundua na kulisimamia hilo na kutoa nafasi kwa Watanzania wanaostahili kushika nafasi hizo kwa sifa stahiki walizonazo. |
36 |
Watu wengi wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba, walipokuwa wakikatiza katika eneo hilo. Ujenzi wa daraja hilo utawezesha watu wengi wa Ruangwa, kuvuka kufuata matibabu katika Hospitali maarufu ya Ndanda wilayani Masasi na wakazi wa Ndanda watavuka na kufanya shughuli za kilimo wilayani Ruangwa. |
37 |
Lakini wakati serikali ikiboresha upatikanaji wa dawa, kwa upande mwingine hali ya utoaji huduma katika baadhi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali za umma, inasikitisha na kutia uchungu, kwa mfano Hospitali ya Sinza Palestina iliyopo wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. |
38 |
Simbachawene aliyekuwa akizungumza kwenye kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na wilaya mjini Dodoma, anawataka waganga hao wakuu kuchukua hatua kali, ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi wanaonyanyasa wagonjwa ili kukomesha tabia hiyo ambayo inachafua sekta ya afya nchini. |
39 |
Pia anataka Hospitali ya Sinza Palestina iangaliwe kutokana na kukithiri kunyanyasa wagonjwa na hata miili ya watu waliofariki pindi wanapotaka kuchukuliwa na ndugu zao, ambapo wamekuwa wakitoa lugha chafu kwa ndugu wa marehemu, hali ambayo imekuwa ikizidisha uchungu mara mbili. |
40 |
Anasema ni jambo lisilokubalika kuona baadhi ya watumishi wachache, wanaendelea kuichafua sekta ya afya bila kuchukuliwa hatua. Hivyo, tukio hilo la Sinza Palestina linadhihirisha kwamba kwenye sekta ya afya nchini, bado kuna watumishi wabaya ambao wanachafua sekta hiyo nyeti. |
41 |
Hali kadhalika, wafanye mikutano na wananchi na kuwauliza juu ya utoaji huduma wa madaktari na wauguzi katika maeneo yao. Tuna hakika wananchi hawawaogopi watumishi wazembe, wanyanyasaji na wanaotoa lugha chafu kwa wagonjwa, hivyo watawataja kwa majina na kuomba wachukuliwe hatua kali. |
42 |
Alisema Serikali haitavumilia kuona usimamizi mbovu na utawala wa michezo usiojali maslahi ya Taifa ukiendelea kudumaza michezo nchini. Tunampongeza Waziri Mkuu kwa kauli yake nzito iliyolenga kusafisha uozo ulioko michezoni tukiamini kuwa itachochea hatua ya kujisafisha. |
43 |
Tunasema hayo kwa sababu pamoja na vyama vingine kutotegemea fedha za Serikali, bado vina dhamana kubwa kwa Watanzania wote. Kwa maana hiyo, si haki hata kidogo vyama hivyo kukataa kudhibitiwa katika uendeshaji wakati maslahi ya michezo vinayoisimamia ni ya wananchi wote hata kama si wanachama wake. |
44 |
Tunapongeza hatua hiyo, iliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ambaye alisisitiza kuwa lengo la kuhamishia mahakama huko Ihefu, linatokana na baadhi ya wafugaji kuonekana kuwa sugu wa ulipaji faini kila wanapokamatwa, lakini hawaachi kuingiza mifugo hifadhini. |
45 |
Ikumbukwe kuwa juhudi zilizoanza kuchukuliwa na serikali tangu mwaka jana, tayari zimeanza kuzaa matunda, kama vile baadhi ya wanyama wameanza kurudi katika eneo hilo. Hivyo, kamwe tusiwape nafasi watu wachache, ikiwemo wafugaji jeuri, kuharibu Bonde la Ihefu na Hifadhi ya Ruaha kwa ujumla. |
46 |
Kama ambavyo viongozi mbalimbali wamekuwa wakisisitiza akiwamo Amiri Jeshi Mkuu, kila mmoja ana wajibu kuhakikisha nchi inakuwa salama wakati wote kutokana na mchango na nafasi ya kila mmoja, na hii ndiyo sababu iliyomfanya kusisitiza wanasiasa waepuke kuviingilia vyombo vya dola. |
47 |
Katika hili, kunahitajika mchango na wajibu wa kila mmoja kutambua nafasi yake muhimu katika kulinda na kuimarisha amani ya Tanzania. Tunaungana na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania kusema, vyombo vya Dola viachwe vifanye kazi zake na wanasiasa wasijaribu wala kupewa nafasi ya kuviingilia. |
48 |
Ndiyo maana tunasema, pendekezo la Rais Magufuli la kuongeza siku tano za maonesho katika viwanja hivyo mwaka huu, litakuwa na faida nyingi kwa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuongeza mauzo na manunuzi ya bidhaa mbalimbali, na hasa kupata fursa ya kutosha ya watu kujifunza katika maonesho hayo. |
49 |
Kwa mujibu wa Waziri mwenye dhamana, mwaka huu kila siku ya maonesho imetengwa kwa shughuli maalumu ya kumsaidia mshiriki kujiimarisha kibiashara, zipo siku za mazungumzo baina ya wafanyabiashara, siku za kukutana wafanyabiashara wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na siku ya kujadili bidhaa. |
50 |
Hakuna ubishi kwamba Tanzania tofauti na nchi nyingine za bara la Afrika na mabara mengine, ni nchi yenye sifa ya kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu na pia kimbilio la wengi ambao hali zao za maisha katika nchi zao si shwari kiasi cha kuja hapa nchini kupata hifadhi ya usalama wao. |
51 |
Sifa ya utulivu, amani na mshikamano wa Watanzania bado ipo lakini jambo moja la msingi na ambalo lilizungumzwa sana na viongozi wetu wa serikali, dini na jamii katika siku hizo mbili za mapumziko ya juzi na jana ni hali ya watu kuwa katika mazingira tatanishi katika wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani. |
52 |
Hakuna ubishi kwamba rasilimali ya ardhi duniani kote, inapewa umuhimu wa pekee kwa sababu ndiyo kunakuwezesha kufanya miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo, ujenzi wa viwanda, makazi, miundombinu, shule, vyuo na mambo mengine makubwa ya kujiendeleza na kujiletea maendeleo endeelvu. |
53 |
Jeuri hii ya kumiliki ardhi yetu ndiyo inayotufikisha salama sasa kuweza kusimamia rasilimali zetu ikiwa ni pamoja na madini, gesi na nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa, kiasi cha kuwa katika hali nzuri ya kuweza kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwa sababu ardhi tunayo ya kutosha. |
54 |
Ameomba Watanzania wampe ushirikiano na kumuombea kwa Mungu, ashinde vita dhidi ya wezi hao kwa sababu anapambana nao kwa faida ya wote. Alisema hayo katika viwanja vya Bwawani wilayani Kibaha mkoani Pwani akiwa katika siku ya ziara ya kikazi ya siku tatu, inayomalizika leo. |
55 |
Michuano ya Ndondo inakutanisha timu za mtaani ambako wananchi wengi hupenda kuangalia timu zinazofanya mazoezi na kucheza mechi katika maeneo wanakoishi. Ni wazi michuano hii inaendeleza uhusiano mwema wa wananchi kupitia michezo na kuongeza ushirikishwaji katika maendeleo. |
56 |
Kama ilivyo kwamba kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani, wapo baadhi ya Watanzania waliojivisha ukenge na kuendelea kuibeza Kamati na kuwajaribu kuwakatisha tamaa Watanzania na kuwasaliti katika suala hili wakipambana kuwalinda wezi wa rasilimali za taifa. Hata hivyo, sauti ya Mungu. |
57 |
Wakati bajeti ikiwasilishwa bungeni, wabunge na hata wananchi katika maeneo yao mbalimbali walikuwa wakishangilia kile walichokiona kuwa ni bajeti bora na hata baada ya hapo, wananchi wa kada mbalimbali wameendelea kuipongeza bajeti hii ya pili katika uongozi wa Rais John Magufuli. |
58 |
Sambamba na hayo, bajeti hiyo imewatambua rasmi wafanyabiashara ndogo wasio rasmi maarufu kama machinga, mamalishe, wauza mitumba, kuondoa ushuru wa forodha kwenye malighafi na vifaa vinavyoagizwa nje kwa ajili ya kuunganisha na kutengeneza vifaa ambavyo ni mahsusi kwa ajili ya matumizi ya walemavu. |
59 |
Sisi tunasema, tunampongeza kwanza Rais Magufuli kwa kufanya uteuzi unaozingatia zaidi maslahi ya taifa, na sio maslahi ya chama chochote cha siasa wala mtu binafsi. Tunasema mwendo huu utazidi kuliunganisha taifa na hatimaye taifa la Tanzania litakuwa na ajenda za pamoja kitaifa. |
60 |
Kadhalika, tunampongeza Mghwira kwa kuteuliwa na kuapishwa, kuanza kazi sambamba na kauli aliyoitoa baada ya kuapishwa kuwa yeye si mpinzani wa maendeleo. Pamoja na hayo, tunapenda kumkumbusha Mghwira hatua ya kuteuliwa, inaonesha kuwa Rais ameridhika na uwezo wa kazi na uadilifu kwa taifa. |
61 |
Tunasema hivyo tukizingatia kuwa jana moja ya magazeti ya kila siku nchini, liliripoti kuwa ugonjwa wa kipindupindu umeanza kuibuka katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam na kusababisha watu tisa kuwekwa karantini katika Zahanati ya Makurumla baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo. |
62 |
Ndiyo maana tunasema, usafi unaosisitizwa na Serikali ufanyike kwa dhati na kila mmoja aufanye kwa manufaa yake na taifa kwa jumla na sio kwa kuogopa mkono wa sheria. Uwekwe utaratibu mzuri zaidi wa kukusanya taka na kuzizoa mapema ili kuepusha hatari hizo za wazi na ambazo zinzaweza kudhibitiwa. |
63 |
Tunaipongeza Serikali ya Rais Magufuli kwa kuwa mfumo huo wa ukusanyaji kodi za Serikali, utaondoa na kumaliza malalamiko yaliyokuwepo awali kwa wakusanya kodi na walipa kodi, waliokuwa wakisema wanatozwa kodi kutokana na makadirio ya juu kuliko halisi halisi ya biashara na mapato yao. |
64 |
Moja ya mapungufu hayo ni mwanya wa mlipa kodi kutoa taarifa za uongo, hivyo kufanyiwa makisio ya chini, jambo ambalo ni mwanya wa kuiba pato la Taifa. Mapungufu mengine yalikuwa mwanya mkubwa wa mlipakodi na mkusanya kodi, kushirikiana kudanganya Serikali kupitia rushwa. |
65 |
Hili pia litaondoa kero kwa watumiaji wengine, wakiwamo watumiaji wa njia na barabara zinazofungwa kwa biashara ya wamachinga katika mitaa kadhaa ya miji mingi. Miundombinu hiyo ikiimarishwa na kuboreshwa, itaimarisha usalama wa kimwili na kibiashara kwa wafanyabaishara hao. |
66 |
Wakati tukirejea pongezi zetu kwa Serengeti Boys kwa mafanikio waliyopata Gabon, tunapenda kuungana na Waziri Mwakyembe kuomba wadau mbalimbali wenye uwezo au fursa za kuwatafutia vijana hao nafasi za kupata mafunzo zaidi kwenye timu kubwa nje ya nchi, waunge mkono jitihada hizi za Mwakyembe. |
67 |
Lengo la hatua hiyo ni kubaini kama wana ebola au dalili zake kwa kuwapima joto lao la mwili na hivyo kudhibiti wasiueneze na pia kujikinga. Tunaipongeza Serikali kwa kuchukua hatua za haraka kudhibiti kuenea kwa ebola kwa kupima wageni wote wanaoingia na kukinga wenyeji. |
68 |
Ndiyo maana tunasema, kwa kadiri itakavyofaa, Rais na Serikali yake waangalie pia uwezekano wa kuunda kamati maalumu kushughulikia masuala yote tata katika sekta nyingine mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanayofanya ni kwa ajili ya masilahi ya Watanzania wote na siyo wachache. |
69 |
Jamii ielezwe wazi matibabu na huduma dhidi ya fistula hutolewa bure katika hospitali zote. Ndiyo maana tunasema, wakati tukiadhimisha siku ya fistula jana tatizo hilo sasa liwe ajenda ya Watanzania mahali popote ili kuwapunguzia mateso wanawake kulinda nguvu kazi ya taifa. |
70 |
Kwa msingi huo, tunashauri wakuu wa mikoa, wilaya na viongozi wengine katika ngazi za kiutawala wakisaidiana na waganga wakuu na wafawidhi, kuanza kutoa elimu sahihi na ya kutosha katika maeneo yao kwa nchi nzima kuhusu dalili, madhara na namna ya kujikinga au kutibu ugonjwa huo. |
71 |
Ni kweli kwamba bado hatujafikia lengo letu lakini hatuna budi kujidai pia kwamba tupo katika njia sahihi ya kuelekea tunakotaka kwenda na hivyo kila mmoja wetu kwa nafasi yake bila kufanya ajizi aweze kushiriki kikamlifu katika mikakati ya kuelekea katika uchumi wa viwanda. |
72 |
Serikali, wanasiasa na wananchi kwa ujumla wao wawe tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa kuendelea kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi yetu ili waje kwetu kuwekeza katika sekta hii ambayo inaonyesha kila dalili ya kuweza kuwapatia watu wetu suluhisho la tatizo la ajira. |
73 |
Pamoja na kupongeza Benki kuu kuchukua maamuzi hayo mapema kuokoa fedha za wananchi kwa kiasi kinachowezekana, sisi tunaona ipo haja kwa Benki kuu Kutoa taarifa ya ujumla kuhusu hali ya kifedha katika benki zetuj ili kuondokana na hofu ambayo inaweza kuwakumba watu wa kawaida. |
74 |
Habari hiyo ikaeleza kwamba baada ya kuulizwa, mtu huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho kilichotajwa hapo juu, akasema silaha hiyo pamoja na risasi, ni mali ya baba yake. Kutokana na tukio hili, tunapenda kushauri mambo kadhaa yatakayosaidia kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini. |
75 |
Kadhalika, tunapenda kulishauri Jeshi la Polisi kuhakikisha linaendelea kusimamia na kutoa au kuruhusu mtu binafsi kumiliki silaha za moto baada ya kujiridhisha kuwa ni mwadilifu, mwenye akili timamu, makini na aliyepata mafunzo ya kutosha kumiliki na kutunza silaha hizo. |
76 |
Tunaamini hili likifanyika, litaepusha madhara mbalimbali yakiwamo ya uwezekano wa watoto kuchukua silaha hizo na kuchezea, hivyo kuhatarisha maisha yao wenyewe na ya watu wengine au, kutoa mwanya silaha hizo kuangukia mikononi mwa wahalifu hususani majambazi na majangili. |
77 |
Ni dhahiri mafanikio yaliyopatikana kwa kuwa na mikoa mitatu ya kipolisi katika Jiji la Dar es salaam yatapelekwa katika mkoa wa Kipolisi Rufiji ili kuona kwamba wananchi wanaendelea na shughuli zao bila kuogopa wakora wanaoleta mtafaruku katika maisha ya watu mbalimbali. |
78 |
Tunaamini kama anavyoamini kamishina kuwepo kwa sera kungesaidia kurejesha thamani ya bima miongoni mwa wananchi walikokata tamaa na hivyo kuanzisha mikakati ya watu kutambua na kuithamini bima katika sekta ya afya na yenyewe kuisaidia nchi katika kuhakikisha afya bora kwa wote. |
79 |
Sekta ya habari imepanuka na kuongezeka kutoka zile za kimapokeo ya magazeti, radio na televisheni hadi kwenye mitandao ya kijamii ambayo nayo inatoa habari kwa jamii kwa haraka zaidi kuliko vyombo hivyo vya mapokeo ingawa umuhimu wa vyombo hivyo uko paleplae na unazidi kuongezeka. |
80 |
Sisi tunatumia maadhimisho na fursa hii kukumbushana kuwa, Tanzania hivi sasa vipo vyuo vya ngazi mbalimbali kuanzia ya vyeti, diploma, digrii na kuendelea juu zaidi. Mwanafunzi kwa sasa halazimiki kusoma akiwa muda wote shuleni, bali anaweza akaendelea na masomo huku akifanya kazi zake pia. |
81 |
Ni wazi kuwa hatua hizo kubwa alizotangaza, zimekuwa zikisubiriwa kwa muda mrefu na wakulima nchini ili kuwaondolea kero. Tunaamini kuwa kufutwa kwa tozo hizi, ambazo zilikuwa kero kubwa, ni utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli kwa wakulima nchini. |
82 |
Katika hili tunaipongeza Serikali hasa tukikumbuka pia namna ilivyotangaza hadharani kuwa baada ya mambo hayo kukamilika, kutakuwa na ongezeko la mwaka katika mishahara ya wafanyakazi huku katika mwaka huu wa fedha, watumishi wakianza kupandishwa vyeo na madaraja ya kazi. |
83 |
Katika maadhimisho haya yanayofanyika mwaka huu kitaifa mkoani Kilimanjaro huku mgeni rasmi akiwa Rais John Magufuli, tunawapongeza wafanyakazi wote waliojitoa kwa moyo kufanya kazi kwa uadilifu katika mazingira na maeneo ya kazi huku wakizingatia kuwa haki siku zote huendana na wajibu. |
84 |
Kwetu sisi maadhimisho ya mwaka huu ya Mei Mosi, yameangukia katika kipindi kinachohitaji tafakuri ya kina ili kurekebisha makosa na "kuzisafisha siku za usoni." Gazeti hili katika toleo la jana, lilichapisha majina yote yaliyopo kwenye ripoti ili umma uwatambue kama alivyosema Rais. |
85 |
Funzo lingine ni kuhakikisha anafanya kila jambo kwa njia halali iliyojaa uaminifu na uadilifu ili Tanzania isiwe kichaka la wahuni wanaoishi kwa njia za mkato, bali waadilifu na wanaozingatia kazi kwa juhudi na maarifa huku wakizingatia kuwa haki na wajibu vinategemeana kama kuku na yai. |
86 |
Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli imetoa umuhimu wa pekee katika matumizi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa shughuli za kitaifa na kimataifa, ikiwa ni msukumo mwingine wa kuhakikisha kwamba lugha hiyo inazidi kupaa katika nyanda za kitaifa na kimataifa. |
87 |
Tunapenda kutoa pongezi maalumu kwa Rais wetu kwa maamuzi yake ya makusudi ya kukuza lugha yetu lakini pia kwa kuonesha njia ya kutaka kuwapeleka walimu wa lugha ya Kiswahili kwenda kufundisha majirani zetu wa Rwanda ambao tayari wameshatoa maamuzi ya kutumia Kiswahli kufundishia katika shule zao. |
88 |
Hakuna ubishi kwamba Tanzania ndiyo nchi ambayo iko katika nafasi nzuri ya kutoa walimu wazuri kwenda kufundisha lugha hiyo popote duniani kuliko nchi nyingine yoyote barani Afrika kutokana na sababu zilielezwa hapo juu na ambazo hakuna nchi nyingine yenye kubarakiwa kwa fursa hizo. |
89 |
Tumaini ushirika wao umelenga kuhakikisha kwamba wanashirikiana na wadau wote muhimu ili kuhakikisha kuwa mtiririko wa maji kuelekea mabwawa ya Mtera na Kidatu ambayo ni tegemeo kubwa kwa uzalishaji wa umeme unaimarika na kuwa bora ili kuondokana na tegemezi la umeme wa mafuta. |
90 |
Ni kweli kama alivyosema, Profesa Assad kuna ulazima wa kufanya juhudi za makusudi kuinusuru Tanzania na bei ghali ya nishati ili uwekezaji uwe nafuu na Tnaesco yenyewe kupumuia ili kufikiria vyanzo zaidi vya nishati na hivyo kusonga mbele katika ndoto ya kuwa na Tanzania ya viwanda. |
91 |
Simbu ameanza kuturejesha katika furaha, kwani ameonesha mwelekeo wa kufanya vizuri na sasa Jumapili ana kibarua kigumu katika London Marathon. Mafanikio ya Simbu yamekuja baada ya Kampuni ya Multchoice Tanzania kujitokeza kumdhamini katika maandalizi yake pamoja na kumpatia mshahara kila mwezi. |
92 |
Rais Magufuli akizungumza na majaji hivi karibuni aliwataka kuwa makini kwa kuwa kesi zinazopelekwa mahakamani, serikali imekuwa ndiyo inayopoteza kwa kuwa ama na ushahidi hafifu au kutokuwepo na ushahidi kabisa, hivyo kuifanya serikali mara kwa mara kulipa gharama za kesi hizo. |
93 |
Kairuki akaongeza kwamba kutokana na kuimarika kwa kitengo cha ufuatiliaji na urejeshaji wa mali, Takukuru imefanikiwa kutaifisha nyumba sita na kutaifisha pia magari manne, mawili aina ya Toyota Chaser, jingine Toyota Land Cruiser na Mitsubishi Fuso yaliyopatikana kwa njia ya rushwa. |
94 |
Kwamba nchi yetu imekuwa kisiwa cha amani kwa muda mrefu, hivyo mauaji hayo, hayavumiliki na jamii ya Watanzania. Tunaunga mkono kuwa hali si nzuri, kwani matukio ya uhalifu yanazidi kuongezeka mijini na vijijini kila siku na yapo katika sura mbalimbali, hivyo kuhatarisha amani na umoja. |
95 |
Aidha, tunaunga mkono kauli za viongozi wa dini za kutaka Watanzania kufuata maelekezo ya serikali ya kukata bima ya afya, kwa kuwa bima ya afya ndio mkombozi wa watu wengi, hasa wenye kipato cha chini. Kwa sasa matibabu yana gharama kubwa na watu wengi wamepoteza maisha kwa kukosa bima ya afya. |
96 |
Kitu kingine walichosisitiza viongozi wa dini ni kuliombea taifa, liendelee kudumisha umoja na amani. Madhehebu yote ya dini nchini, yanatakiwa kuliombea taifa kila siku bila kukoma ili liweze kusonga mbele kiuchumi na kijamii na kujiepusha na umwagaji damu usiokuwa wa lazima kwa wananchi wake. |
97 |
Hapa tungependa kutoa angalizo kwa walezi na wazazi kuwa makini na watoto wao wanapokwenda katika sherehe mbalimbali katika siku hizo nne za mapumziko. Kuna tabia au utamaduni wa kuwaacha watoto kwenda mbali ya mahali wanapoishi kwa lengo la kushirikiana na wenzao katika sherehe hizo. |
98 |
Tungependa kutoa mwito kwa wazazi na walezi kujitahidi katika uangalizi wa watoto katika kipindi hiki ili basi sherehe hizo zimalizike salama na hatimaye kuendelea na shughuli nyingine za ujenzi wa taifa na watoto, ambao sasa wako likizo, warejee shuleni baada ya mapumziko. |
99 |
Hakuna ubishi kwamba kama hali hiyo haitatafutiwa suluhisho la kudumu watoto wengi wa kike katika wilaya hiyo wataendelea kukatishwa tamaa katika harakati za kutimiza ndoto zao za kuwafikisha katika elimu ya juu na kupata ujuzi wa kuwasaidia maishani mwao kama ilivyo wenzao wa kiume. |
100 |
Tatizo la ukosefu wa hosteli au mabweni ya wasichana halipo katika jimbo la Busega peke yake bali pia katika majimbo na mikoa mingine hapa nchini. Hali kama hiyo ya wasichana kuingia katika vishawishi vya ngono na hatimaye kuishia kupata ujauzito lipo pia katika maeneo hayo mengine. |
101 |
Ukweli ni kwamba hali ndani ya Bunge hilo, haikuwa shwari kwani kutokana na kutofautiana kwa hoja, kuliibuka vurugu huku baadhi ya wabunge wakisikika wakitoa maneno yasiyo na staha dhidi ya wabunge wengine, lakini pia kiti cha Spika kilichokuwa kinaongozwa na Spika mwenyewe Job Ndugai. |
102 |
Ni wazi kuwa wakati umefika wa wabunge hawa ambao ni wawakilishi wa wananchi, kuonesha mfano wa nidhamu wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge na kujadili kwa hoja mada zinazowasilishwa kwenye chombo hicho badala ya kutoa lugha zenye matusi zinazokaraisha na kukiharibia sifa chombo hicho. |
103 |
Hapa tungependa kuwakumbusha Watanzania wanaoshiriki katika Wiki ya Ufaransa kujifunza kwa bidii juu ya yale ambayo wanaweza kuyachukua na kuyatumia katika suala zima la ujenzi wa viwanda nchini na kujiweka katika hali ya kuwa washiriki katika juhudi hizo badala ya kuwa watazamaji. |
104 |
Tunatoa changamoto kwa Taasisi ya Sekta Binafsi na wataalamu wengine mbalimbali wanaoshiriki katika shughuli za Wiki ya Ufaransa kutumia nafasi hiyo ya aina yake kama darasa la kujinoa na kujiweka tayari kushirikiana kwa hali na mali na wawekezaji watarajiwa kutoka Ufaransa katika ujenzi wa viwanda. |
105 |
Kama alivyosema Makamu wa Rais, Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye fursa nyingi za uwekezaji. Tunaungana naye kuwakaribisha Wafaransa kuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini kwa kuwa haina matatizo wala migogoro ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa mali zao watakazowekeza nchini. |
106 |
Mipango ya bajeti imewekwa wazi kwa kila mbunge kuweza kuiona na kuchangia na hata kutoa changamoto dhidi ya yale ambayo ni wazi yanaweza kukwamisha kufikia lengo lakini changamoto hizo zisitufikishe katika hali ya kutuingiza katika mifarakano isiyokuwa na tija kwa taifa letu. |
107 |
Katika hili Bunge pia lichukue wajibu wake wa kuisimamia serikali ili ikabiliane vilivyo na maofisa wa serikali wasio waaminifu na wazembe ambao kutokana na utendaji wao usiofuata uwajibikaji waweze kuchukuliwa hatua stahiki kwa matendo yao yanayopingana na majukumu yao kikazi. |
108 |
Uzito huo uliwekewa mkazo wa aina yake pia pale serikali ilipoamua kwa makusudi kutumia Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kufundishia katika ngazi ya shule ya msingi hivyo kuwaweka watanzania karibu zaidi na lugha hiyo siyo tu kwa kuzungumza bali pia kwa kuisoma na kuandika. |
109 |
Sisi tunasema, wanaoitazama bajeti hii kwa jicho la upungufu, hawajatazama vizuri kwa kuwa kitendo cha Serikali kuweka kipaumbele katika ujenzi na uimarishaji wa miundombinu, ni kielelezo na njia sahihi kuelekea kukua kwa uchumi na huduma bora za kijamii kupatikana na kuwafikia wanyonge. |
110 |
Gharama hizo zitaelekezwa katika huduma nyingine za kijamii. Matumizi ya reli katika usafirishaji ni ya uhakika, kwa kiasi kikubwa na kwa gharama nafuu hivyo, kupunguza gharama ya usafirishaji bidhaa na huduma hali inayohitimishwa na gharama ndogo za huduma za kijamii. Vivyo hivyo katika ndege. |
111 |
Kwa kuwa na shirika imara la ndege tunajiweka katika nafasi ya kutoa usafiri wenye kasi na uhakika kwa watu wenye uwezo na wanaotaka kasi katika shughuli zao za ujasiriamali na uwekezaji, ili waweze kuwekeza zaidi kutokana na kuwa na uwezo wa kusafiri eneo lolote la Tanzania kwa kasi wanayoitaka. |
112 |
Kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kwamba wabunge ambao ndio wanaoipitisha, kuangalia kwa makini namna ya kufanikisha bajeti hiyo na kuisaidia serikali kuweza kukusanya fedha hizo kwa ajili ya kuendelea kujenga misingi ya uchumi madhubuti tukielekea kwenye uchumi wa kati. |
113 |
Kuendesha bodaboda ni kazi kama kazi nyingine yoyote inayomletea kipato halali mwananchi yeyote na kila kazi pia ina sheria na taratibu zake. Hakuna ubishi kwamba wananchi wanahitaji usafiri wa kuwafikisha maeneo mbalimbali lakini pia na wenye bodaboda wanahitaji kipato halali cha kuendesha maisha. |
114 |
Wote wanahitajiana lakini pia hawana budi kutoa huduma hiyo kwa usalama kwa wateja wao. Ni vizuri kuwakumbusha wanaofanya biashara hiyo kupata mafunzo ya uhakika ya kazi hiyo ili nao waweze kuifanya kwa uhakika na ufanisi badala ya kuwa shari na maudhi kwa wananchi wengine na serikali. |
115 |
Ziara hiyo ya Spika Ndugai imetanguliwa na ile aliyofanywa na Rais, John Magufuli wiki iliyopita ambapo alibaini kuwapo kwa makontena yaliyokuwa yamekwishafungwa tayari kusafirishwa kwenda nje ya nchi licha ya awali kuwapo kwa agizo lake la kutaka usafirishaji huo usitishwe. |
116 |
Makocha wa timu hiyo wameahidi timu yao kufanya vizuri katika michezo tofauti tofauti na kuiletea heshima Tanzania. Pia Mtaka aliwataka wanariadha kwenda kushindana kwa moyo na kutojaribu kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, kwani kufanya hivyo kutaliletea taifa aibu na sifa mbaya. |
117 |
Kufanya vizuri kwa wanariadha wetu pia kutawasaidia kufuzu kwa mashindano mbalimbali yajayo ya kimataifa kutegemea na muda watakaokimbia. Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ikifanya vibaya katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya riadha wakati huko nyuma tuliwahi kuwika katika mchezo huo. |
118 |
Akasema Jeshi la Polisi halipaswi kuogopwa na raia mwema, ni rafiki kwa kila Mtanzania mwema ambaye ana uzalendo wa dhati na nchi yake na kuongeza kwamba jeshi ni rafiki wa wananchi, hivyo wananchi wanapaswa kuwa karibu na Jeshi kwa kuwa hao ndio walinzi wa wananchi pamoja na mali zao. |
119 |
Kwa ujumla, athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa kwa jamii kuliko faida zake. Kwa kutambua hilo, ndiyo maana tunathubutu kuwaunga mkono vijana waliojitokeza kumpongeza Rais Magufuli katika juhudi zake za kutaka kuwaokoa vijana dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya. |
120 |
Tunaamini kama vijana zaidi na jamii itazidi kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa na Rais Magufuli, ipo siku Tanzania itabaki salama, lakini kama wakiachwa wachache wapambane, hakika hakutakuwa na mwisho mwema katika vita hii, kwani ni dhahiri wenye nia njema watashindwa. |
121 |
Aidha, kwa upande mwingine, dawa za kulevya husababisha mfumuko wa bei unaotokana na fedha za biashara hiyo kuingizwa kwenye mfumo halali, hivyo kuwaongezea wananchi mzigo wa mfumuko unaojitokeza. Kijamii, dawa za kulevya zimeendelea kusababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii. |
122 |
Kwa ujumla, athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa kwa jamii kuliko faida zake, ndiyo maana, bila ya mashaka, tunathubutu kuwaunga mkono na kuwapongeza Umoja wa Mameya wa Majiji na Manispaa kuunga mkono vita iliyoanzishwa na Rais Magufuli dhidi ya dawa za kulevya. |
123 |
Sisi tunasema, tunapongeza kwani hatua hii ni kichocheo cha wanafunzi kujifunza na kuiva sawia ili kwenda sambamba na uhalisia wa maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayopiga hatua kwa kasi duniani kwa kuchukua hatua za makusudi kuwaandaa wataalamu wetu kuanzia ngazi hiyo. |
124 |
Msemaji wa Wizara ya mali asili na utalii, Dorina Makaya amesema madai haya "si ya kweli" kinachoendelea ni uchomaji wa kawaida wa awali ambao unaoendelea kwa awamu, linalofanywa lina lengo kuzuia majanga ya moto kutoka nje ya hifadhi ambayo yanaweza kufikia ndani ya hifadhi. |
125 |
Mwanamume huyo alikamatwa Jumapili ambapo inadaiwa alipatikana akimchuna ngozi paka. Gazeti la Star linasema mwenyewe alikiri kupika sambusa akitumia nyama hiyo. Taarifa kwenye vyombo vya habari Kenya zinasema mwanamume huyo alikiri kuuza nyama ya paka zaidi ya elfu moja mjini humo tangu mwaka 2012. |
126 |
Namna na sababu ya kupewa sumu hiyo bado haijawekwa wazi lakini Shelutete anasema uchunguzi bado unaendelea. Baada ya simba hao kufa, watuhumiwa wa tukio hilo wanadaiwa kukata mikia na miguu yao na kuondoka nayo, jambo ambalo kwa mujibu wa polisi linadaiwa kuongeza walakini juu ya tukio hilo. |
127 |
Nchi wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia. Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka. |
128 |
Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema kuwa hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote. Shirika la Afya duniani sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha. |
129 |
Lakini mpango huu mpya utalenga kuwafundisha watoa huduma wa afya jinsi ya kushughulikia mtu aliyeumwa na nyoka na elimu ya huduma ya kwanza kwa jamii iliyo hatarini. Kila mwaka zaidi ya watu laki moja hufa duniani kutokana na kuumwa na nyoka asilimia 20 kutoka barani Afrika. |
130 |
Afisi ya maswala ya kigeni imesema kuwa inazisaidia familia hizo. Pia imesema kuwa inawasiliana kwa karibu na mamlaka ya DR Congo. Vyombo vya habari vinasema kuwa afisa aliyepigwa risasi hadi kufa alikuwa mwanamke huku raia hao wa Uingereza wakitekwa pamoja na dereva wao raia wa Congo. |
131 |
Licha ya serikali mkoani Lindi kuweka sheria ya kuwataka wanunuzi wa zao la ufuta kutoa ufuta wao ndani ya siku saba baada ya kununua, bado wanunuzi hao wameendelea kuweka ufuta wao katika maghala ya vyama vya msigi. Hatua hiyo imesababisha kuwapo kwa mlundikano mkubwa wa ufuta katika vyama hivyo. |
132 |
Mwaka 1972, Amin aliamuru kufukuzwa kwa watu wa jamii ya Asia, wengi wao wakiwa Wahindi, kutoka nchi hiyo ya Afrika Mashariki, akisema alitakwa kuurejesha uchumi mikononi mwa wenyeji. Sehemu kubwa ya mali walizonyanganywa zimerejeshwa kwa wamiliki wake wa awali chini ya utawala wa Rais Museveni. |
133 |
Miongoni mwa kashfa ambazo Waziri Ndalichako alikutana nazo ni hatua ya uongozi "kuwafaulisha" wanafunzi 204 wa kozi ya stashahada ya elimu bila ya mitihani yao ya mwisho kusahihishwa na wahadhiri wao ambao wako kwenye mgomo kutokana na kudai mishahara yao kwa zaidi ya miezi minane sasa. |
134 |
Kwa kawaida anahamishwa na mshahara wake kutoka alikokuwa, kwa maana kwamba analipwa sawa na huko alikokuwa na nyongeza ya posho kibao juu yake. Nape atakuwa analifahamu hili, amekaa pale ofisi ndogo za makao makuu Lumumba kwa miaka kadhaa sasa, anajua vizuri habari hii. |
135 |
Lina madhara makubwa, ni janga la kiuongozi kwa sababu anayesema uongo akiwa amekalia ofisi ya umma anawasilisha taswira moja wazi, kwamba si mwaminifu, na asiye mwaminifu hawezi kusimamia ofisi ya umma. Inawezekana sana hili ndilo tatizo letu kama taifa, kuwa na viongozi wasiosema ukweli. |
136 |
Kila kisa huwa na ujumbe fulani na kuna matukio yenye maudhui mchanganyiko. Kwa tafsiri yangu, inayoweza kutofautiana na yako na ya mwenzako, filamu ya ziara ya Al-Adawi imeonyesha ukomo wa fikra kwa viongozi wetu. Wamebanwa katikati na ufisadi kiasi kwamba hawawezi kujinasua. |
137 |
Hao hakuna sababu ya kuwanyima sifa zao. Sifa hizo ni dhahiri zinaenda sehemu stahili, lakini anayesifiwa anazipokeaje? Hilo ndilo tatizo la wachezaji wetu na timu kwa ujumla. Timu zinacheza mpira vichwani kabla hata ya kuingia uwanjani huku zikiamini sifa ndizo zinazocheza. |
138 |
Wiki iliyopita niliandika kuhusu kutoona umuhimu wa Kombe la Kagame kuchezwa Tanzania kwa miaka miwili mfululizo, kwani hakuna mantiki yoyote ya kufanya hivyo zaidi ya kudidimiza soka letu. Leo hii tunaona kwani timu zetu hazijiandai ipasavyo na hali hiyo ya kutetea bendera ya Tanzania. |
139 |
Huu ni upuuzi unaoendekezwa bila sababu ya msingi, kubadilika ni muhimu kwa kila mdau wa soka ili Tanzania isonge mbele. Kila siku tunajidanganya na Simba na Yanga kuwa zitakuza soka letu, hakuna hizo zipo kuteka akili zetu na kuamini hata zikija Real Madrid na Barcelona zitafungwa tu. |
140 |
Maamuzi mengi ya klabu hizo ni zimamoto, viongozi wengi wapo kwa ajili ya kujifurahisha tu siyo kuleta maendeleo. Katika Kombe la Kagame, timu nyingi zinaonekana kujipanga zaidi ili kutwaa ubingwa, Simba na Yanga zenyewe zinatumia muda mwingi kuwazungumzia wachezaji inao wasajili. |
141 |
Yanga imemsajili Yondan kutoka Simba na wakati huohuo ipo mbioni kumtwaa Okwi, kazi ipo hapo. Viongozi wapo tayari kumwaga hata mabilioni ya shilingi ili tu kubakisha wachezaji hao katika timu wazitakazo. Hao, hawajuhi lolote kuhusu maandalizi ya timu zao katika michuano mbalimbali. |
142 |
Kombe la Kagame linaumbua usajili wa Simba na Yanga uliokuwa unafanywa kilazima na vibosile ili tu kujihimarishia tawala za uongozi wanazojilimbikizia ndani ya klabu hizo. Dawa yao pekee iliyobaki sasa baada ya mambo kuwashinda ndani ya uwanja ni kucheza soka nje ya uwanja. |
143 |
Na hata kama wangekaa kwa muda mrefu na timu hizo, timu ambayo kocha hakuisajili hawezi kupata kikosi cha kwanza haraka, nje ya hapo atakuwa anabahatisha kupanga kikosi na hata ushindi utakuwa wa bahati. Azam yenyewe ina mfumo maalum wa usajili hadi kutema wachezaji lakini siyo Simba na Yanga. |
144 |
Ni hao hao wanaolaumu magazeti hayo hayo kwa kuzisifia timu hizo pindi zikifanya vibaya. Shabiki huyo naye anahusika katika kuiharibu klabu hizo, kwani anaamini habari nzuri ni ile inayozihusisha timu hizo. Hakika Simba na Yanga zimebebwa mno na magazeti na sasa zinayadhalilisha magazeti hayo. |
145 |
Kwa ufupi, ofisa huyu alitumia fedha nyingi kununua gari kongwe, ununuzi usiotakiwa kisheria serikalini. Utasikia jengo la serikali limekodishwa kwa mwekezaji au mtu binafsi tu pasina kufuatwa utaratibu wa manunuzi unaohitaji sheria ifuatwe na kila anayetaka aombe rasmi. |
146 |
Pengine ni kwa kufukuza watumishi wenzao bila ya kuzingatia kanuni za utumishi, ikiwemo kumpa mtumishi mtuhumiwa nafasi ya kujitetea kabla ya kuadhibiwa. Wapo viongozi serikalini ambao wamegawa zabuni kwa njia ya upendeleo baada ya kuwa wamepata malipo haramu kwa waliopewa zabuni husika. |
147 |
Bali wapo watendaji waliotumika kuvuruga uchaguzi na hivyo kusababisha wagombea walioshindwa kutangazwa kuwa wameshinda. Tena, katika mwenendo kama huo, matokeo ya uvurugaji huo yamesababisha fadhaa kubwa katika nchi ikiwemo machafuko na vifo vya raia waliokuwa wakipinga uvurugaji. |
148 |
Bila ya shaka yoyote, mfanyabiashara huyo alifanikiwa baada ya kuhonga maofisa wa ngazi ya juu wa serikali waliokuwa na dhamana. Kwa upande mwingine, kuna mazingira ya rushwa na ufisadi kukuta mtumishi wa umma anamiliki mali za thamani kubwa isiyolingana na kipato chake. |
149 |
Huo ni ufisadi. Sasa yote haya ni uthibitisho wa jinsi rushwa na ufisadi vilivyoenea katika sekta ya utumishi wa umma. Mdudu huyu amekuwa akiumiza sana haki za watu. Haki zimekuwa hazipatikani na mara chache zinapopatikana, huwa ni baada ya wananchi kuhonga maofisa wa serikali. |
150 |
Wakaanza kulipana. Kwa watu wenye uelewa wa shughuli za bima, wanajua haya madai ni hewa. Wafanyakazi waliosimamishwa kazi lakini wakabaki wanalipwa nusu mshahara kwa zaidi ya miaka kumi, walikataliwa kulipwa. Wale waliofunguliwa kesi feki lakini wakashinda, nao walikataliwa kulipwa. |
151 |
Mwaka huo, miili ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka wilaya ya Ulanga waliochinjwa kwa risasi ya polisi ilitupwa. Huko pia ndiko Dk. Ulimboka alitupwa baada ya kupigwa karibu ya kufa. Katika sakata hili la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka mmoja wa watuhumiwa ni serikali yetu. |
152 |
Ikiwa vyombo vinavyotamkwa kuwa huru na katiba haviko huru, jeshi la polisi ambalo ni sehemu ya serikali litapaje uhuru wa kuichunguza serikali? Si muda mrefu tumesikia kilio cha jaji mkuu kilichodai uhuru wa mahakama haupo kwa sababu watendaji wa serikali wamo ndani ya tume za utumishi wa mahakimu. |
153 |
Aidha, jaji mkuu aliyepita, Augustino Ramadhani, aliwahi kusema uhuru wa mahakama unakuwa mashakani endapo fedha za kuendesha mahakama hiyo zimo mikononi mwa serikali. Tumekuwa tukishuhudia ziara za ghafla za wakuu wa dola katika vyombo hivyo na kuashiria kuingilia mhimili huo wa utoaji haki. |
154 |
Tumeshuhudia serikali ikikubali kushindwa mahakamani na kulipa fidia kwa wafiwa wa watu fulani waliokufa katika mazingira ya kutatanisha kama hili la Dk. Ulimboka. Serikali inaweza kuwa tayari kulipa fidia kwa familia ya Dk. Ulimboka kuliko kuendelea kulumbana naye katika mgomo wa madaktari. |
155 |
Ukweli ni kwamba serikali haina miundombinu wala utashi wa kujikamata yenyewe ikiwa mtuhumiwa namba wani. Na kama kuna mtu ndani ya serikali aliyeidhinisha tendo hili lakini bila ridhaa ya wakuu wa serikali, basi imchukulie hatua za wazi ili kujiosha na kashfa hii mbaya. |
156 |
Hapa tunazumgumzia utekwaji wa Dk. Ulimboka kwa mtutu wa bunduki za serikali! Kama hili halifanyiki, ni bora wana harakati wote na wenye maoni tofauti na mfumo wa serikali ya sasa, waanze kutafuta hifadhi za ukimbizi katika nchi nyingine maana yaelekea kilichomtokea Dk. Ulimboka ni tangazo la awali. |
157 |
Yaliyomkuta Dk. Ulimboka yanatia simanzi na majonzi kwa kila atakayeyakumbuka baadaye. Atakayesimuliwa atashindwa kuelewa ni kwa kiasi gani binadamu anaweza kuwa mkatili kwa binadamu mwenzake kiasi hiki! Liwalo na liwe limekuwa blanketi zito jeusi la simanzi; limeufunika gubigubi uso wa nchi yetu. |
158 |
Lakini tunalojua ni kwamba kuna mgogoro mkubwa kati ya madaktari na serikali. Pia tunajua kuwa Dk. Ulimboka ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania na ndiye anaongoza mgomo wa madaktari. Hivyo, kusema Dk. Ulimboka alikuwa katika ugomvi mkubwa na serikali ni sahihi kabisa. |
159 |
Mwanadamu alivyoumbwa na Mwenyezi Mungu ni kwamba, maafa yanapomkuta mtu yeyote, wa kwanza kushikwa uchawi ni yule aliyenaye katika ugomvi wakati huo. Wanaofikiri kuwa serikali ndiyo imetenda unyama huu dhidi ya Dk. Ulimboka, wanafikiri kibinadamu! Kumbe wafikirije? Ni haki yao kufikiri hivyo. |
160 |
Iwe Mabwe-Pande au msitu wa Pande ukiunganisha na polisi vichwani mwa wananchi inaibuka kumbukumbu ya kutisha inayokumbusha tukio la kinyama lililowasibu wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge na dereva teksi wa Dar es Salaam. Waliuawa kwa kupigwa risasi visogoni bila kuwa na hatia yoyote. |
161 |
Kosa likafanyika, polisi wakafungua kesi, wakavuruga ushahidi mahakama ikawaachia washirika wa mauaji ila ikaagiza polisi muuaji akamatwe. Huu ni mwaka wa saba, polisi hawahawa wanaotaka kuchunguza suala la Dk. Ulimboka, wamekwepa kumkamata mwenzao aliyeua wafanyabiashara wale. |
162 |
Huwezi kujivunia madaktari wa Jeshi ambao nao wana wagonjwa wao wa kutosha. Madaktari wa Jeshi hawagomi, lakini ni mshahara upi mkubwa kati ya ule wa kijeshi na wa udaktari? Waliojenga hospitali za serikali wakatenga kuwa hizi zitumiwe na jeshi na hizi zitumiwe na raia walikuwa na fikra kubwa. |
163 |
Je, siyo kweli kuwa ukiwajumlisha madaktari wote, wanajeshi, wa hospitali binafsi na hawa waliogoma nchi bado ina upungufu wa madaktari? Unazibaje upungufu kwa kutumia upungufu? Viongozi wetu wanahangaika sana huku wakifanya kazi ya bure. Umri wa kustaafu ukifika mtu aliyechoka anapumzika. |
164 |
Wamechoka kuona wagonjwa wakifariki kwa kukosa hata oksijen tu! Wamechoka kuwalaza wagonjwa chini au kuwalundika katika kitanda kimoja wenye magonjwa tofauti tofauti. Wamechoka kuwaandikia wagonjwa dawa ambazo hazipo hospitalini lakini kwenye Bohari Kuu ya madawa zipo. Wanaitaka serikali inunue. |
165 |
Ni kwa sababu moja tu, kwamba katika mazingira ambayo umma umekwisha kuamini kwamba Rais Kikwete ni dhaifu, Waziri Mkuu ambaye alitarajiwa afurukute naye amekuwa dhaifu zaidi kuliko hata Rais wake; ni vigumu kuitazama serikali ya awamu ya nne na kushindwa kwake katika mambo mengi bila kumtaja Pinda. |
166 |
Unyenyekevu wake na kujipachika jina la mtoto wa mkulima, kama havibadilishi hali ya mambo serikalini na kuwafanya watu wachape kazi, havisaidii kitu. Kukwepa kuwa mkali na kuamini kwamba muda utapita na kila kitu kitapita, siyo mbinu na mkakati mzuri kwa mwenye nafasi kama ya Pinda. |
167 |
Hebu tujiulize swali la msingi, iweje mtu wa China au Afrika avutiwe na soka ya Ulaya kiasi cha kudharau usingizi wake na kuhatarisha maisha ili tu atazame mechi za nchi za Ulaya? Ni uzalendo au utumwa? Jibu laweza kuwa rahisi, kwamba hakuna soka ya kuvutia katika mabara hayo. |
168 |
Wachezaji wanaolipwa mamilioni ya shilingi ndio wamegeuka chanzo kikubwa cha ajira. Wachezaji wana watendaji kadhaa ambao wamewaajiri binafsi, wana daktari, wanasheria, washauri, madereva, mafundi, watunza nyumba, makocha na hata walinzi ambao kila siku wanawajibika kwa mwanasoka binafsi. |
169 |
Mfano mdogo ni Afrika Kusini na Misri, ambazo angalau wachezaji wananufaika na jasho lao kutokana na malipo mazuri. Kwingine kote kuliko baki ni hadithi na ubabaishaji mkubwa wa harakati za kuinua soka, nchi za Ulaya zimeshatutawala kifikra katika kuamini kila kitu chao ni bora. |
170 |
Kama mtu anataka kuleta maendeleo katika klabu, anawezaje kutumia kiasi cha Sh. 70 milioni kwa usajili huku akikataa katakata kutoa Sh. 30 milioni kwa ajili ya kutengeneza sehemu ya kuchezea kiwanja. Mfano huu unaenda kwa Yanga. Uwanja wao wa Kaunda ni kipara, usiofaa kwa mazoezi ya soka. |
171 |
Alilalamika kuwa serikali hii inataka kulichezea bunge na kuwa yeye binafsi kama sehemu ya uongozi wa bunge hayuko tayari kukubaliana na udhaifu huo. Sikuamini macho yangu wiki iliyopita nilipomwona Ndugai akitokwa na pofu mdomoni kushinikiza Mnyika atolewe nje ya lango la bunge. |
172 |
Huu ni udhaifu mkubwa kwa Ndugai, na sidhani kama nimemtusi kwa kusema hivyo kwa sababu, wiki iliyopita alionekana wazi kutekeleza kitu asichokiamini toka moyoni mwake. Tabia ya viongozi na watendaji wetu kulalamika nyuma ya migongo ya wakuu wao, haiwasaidii wakuu wao wala wao wenyewe wanaolalamika. |
173 |
Kama Ndugai angemuacha Mnyika afafanue kauli yake ilikuwa na maana gani, angekuwa amelitendea haki taifa. Utamaduni wa kutosema kweli au kufumbafumba mpaka kupoteza maana nzima ya kile kinachomaanishwa, inawadhalilisha wabunge wetu bila kubadili hali ya maisha ya wananchi waliowachagua. |
174 |
Nilipata kusema huko nyuma kwamba katika nchi za Kiafrika, ambazo katiba za nchi zimetengeneza marais wenye nguvu kuliko hata wafalme, chochote atakacho Rais huyu huwa. Kwa maneno mengine marais wa Afrika akiwamo wa Tanzania wana madaraka ya kisheria ya kuumba na kufanya lolote. |
175 |
Kuhusu uzalendo, vijana walifundishwa kuipenda nchi, kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya nchi, kuitumikia, kuilinda, kujenga ushirikiano na mshikamano kitaifa na kutotoa siri za nchi. Vijana walifundishwa historia ya nchi, uzuri wa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na ubaya wa ubepari. |
176 |
Mathalani, mimi binafsi ni Muunguja na sina hata damu ya Kipemba, lakini sithubutu kumdharau Mpemba hata siku moja; namchukulia kama ndugu yangu wa kuzaliwa na siyo wa kuungana kama Watanganyika. Hakuna historia inayoonesha kama visiwa hivi viwili viliungana au vilikuwa mbalimbali. |
177 |
Upo hapo? Nasikia ziliandaliwa vocha za malipo, zikaandikwa hundi na kupitishwa zote bila tatizo na kupelekwa benki ambako pesa ziltolewa na kuletwa ofisini kwa ajili ya mgao lakini kumbe ngurumbili mmoja ambaye hakuwamo katika dili hilo alipata taarifa na kumtonya mkuu wa usalama. |
178 |
Jambo la pili nililothibitishiwa ni kwamba Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe ndiye aliyelishikia bango jambo hili la wizi na kwamba sasa hivi viongozi wengine karibu wote wamemgomea na wanadai kuwa eti hakuna pesa zilizoibwa bali eti yalikuwa mandalizi ya safari za rais siku za usoni. |
179 |
Nasikia eti sasa hivi Membe kakalia kuti bovu pale Mambo ya Nje na kwamba kesi hii ya tuhuma za wizi wa pesa ikiisha yeye ndiye atakayebebeshwa lawama na hivyo huenda akang'olewa ili kumrejesha dada yetu Asha-Rose Migiro pale wizarani baada ya kurejea kutoka Umoja wa Maaifa. |
180 |
Nasema tuanzie kipindi cha Mkapa kwa sababu kipindi hicho ndicho mali za umma ziligeuka kuwa mali za ikulu, nyumba za serikali zikawa za watumishi wa serikali, migodi ikauzwa kwa watoto, wakwe, marafiki na wajukuu zao. Tuanzie kipindi hicho hicho kukagua kila safari na kama watu walisafiri kweli. |
181 |
Wala baadhi ya wajumbe wa bodi hawakuwa na taarifa na mkutano huo, na waliousimamia walisema ulilenga kuelimisha umma maazimio ya mkutano wa wadau. Mmoja wa wakurugenzi wa Bodi anatajwa kuwa ndiye aliuitisha na ndiye aliyeratibu ikiwemo kulipia posho za waandishi wa habari walioalikwa. |
182 |
Kwani ni nani anayepaswa kuitisha na kuratibu vikao vya bodi ya wakurugenzi wa mashirika na taasisi za umma? Si ni katibu wa bodi husika? Unapokuta wajumbe wa bodi wanaitisha, kuratibu na kulipia vikao vya bodi ikiwemo kuchapisha maamuzi ya vikao vya wadau wa sekta ya bodi husika, hapo kuna tatizo. |
183 |
Hivi karibuni, Rawlings alihutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Aflao, karibu na mpaka wa Togo, na kusema kwa sasa hakuna mtu anayeweza kuiokoa Ghana kutokana na tatizo kubwa la rushwa na ufisadi isipokuwa mkewe huyo ambaye ni mto wa chifu. Hali hiyo inahitaji kuangaliwa upya. |
184 |
Bob Makani alipewa kazi maalum ya kukipeleka chama mikoa ya Morogoro, Kigoma, Tabora, Singida, Mwanza na Rukwa. Kwa kuwa wakati huo, kuanzisha chama kipya ilionekana kama uasi au uhaini, kwenye mikutano mingi ya hadhara katikae mikoa hiyo, alipokewa kwa matusi na mara nyingine na mawe. |
185 |
Mara tatu Jangwani, nilimsikia Steven Wasira akitoa ahadi ya kufungua mashamba makubwa Kilombero ya kilimo cha mchele. Wasira anajua kuwa mchele haulimwi bali mpunga, lakini kwakuwa alichokuwa akikisema kilikuwa hakitoki kifuani mwake bali mdomoni tu, akawa anasema chochote tu. |
186 |
Aidha, ningependekeza wabunge wastaafu katika wilaya zote nchini, watambuliwe na kuingia kwenye vikao vyote vya chama ngazi ya kata hadi wilaya kutokana na nyadhifa zao walizokuwa nazo huko nyuma. Hatua hii itawafanya hawa wastaafu wajisikie kama bado wanaheshimiwa ndani ya chama. |
187 |
Nani asiyetaka kupeperusha bendera ya nchi? Viongozi wapo tu kwa mujibu wa katiba lakini siyo kwa mujibu wa itikadi za chama. Wengi wamekata tamaa, hawaoni mabadiliko ya kweli yakiwagusa katika maeneo yao ya kazi. Siyo siri, sasa hakuna mikutano ya hadhara inayofanyika tena katika ngazi zote. |
188 |
Mkutano ule, kama ulivyotangazwa na katibu mwenezi wa mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba, uliitishwa kwa lengo la kuwapa wananchi majibu ya kero walizotoa wanachama wa mkoa wa Dar es Salaam katika ziara iliyofanywa na mlezi wao Abdulrahiman Kinana. Huyo alitarajiwa kuwapa majibu. |
189 |
Mawaziri, japokuwa ni kweli wanatoka chama tawala, wanawajibika kwa wananchi wote na si chama peke yake. Hiyo ndiyo sababu mawaziri walijitokeza na harara kujibu shutuma za ugoigoi walizotupiwa na wapinzani wao; na siyo kutoa majibu Kinana alisikia nini kutoka kwa wanachama katika ziara yake. |
190 |
Hivi sasa tunaye kijana Nape Nnauye anayeiongoza idara hiyo. Kuna wanaolalamika juu ya utendaji kazi wake. Ni vigumu kujua kijana huyu anafanya kazi za mezani saa ngapi, anasoma majarida na vitabu saa ngapi, na anajiandaaje kuongea na umma saa ngapi. Ni rahisi kumlalamikia Nape kuliko kumsaidia. |
191 |
Wazee waliotajwa hapo juu ama wamekufa au wamekwisha nguvu. Wengine ni wastaafu au wapowapo. Kizazi kipya cha kuzalisha hoja motomoto hakionekani. Lakini hata hili lina sababau zake. Miaka 50 ya utawala wa chama kimoja haumomonyoi miili tu; unamomonyoa akili na uwezo wa kufikiri. |
192 |
Kama hakukuwepo na mrithishano wa fikra na hasa fikra zinazokua na kunyumbulika; zile fikra endelevu zinazozaa matunda mema wakati wote, basi itafika wakati kutatokea mkwamo. Nilipoongea na Nape alidai, mwenyekiti amelalamika kuwa wapinzani wanaachwa wanapotosha ukweli, kwa hiyo inabidi wajibiwe. |
193 |
Sayi akaamrisha vikombe vile vigawanywe kwa kila mwanafunzi kikombe kimoja halafu akatutangazia kwamba turudi nyumbani kwa sababu Tanganyika ilikuwa imeungana na jirani yake Zanzibar na hivyo siku ile ilikuwa sikukuu. Kutoka pale tilishindana kukimbia kurudi nyumbani na vikombe vyetu. |
194 |
Furaha na hamasa ya kukimbia ilitokana na kupewa kikombe cha plastiki na siyo muungano. Ikumbukwe kwamba wakati ule vyombo vya nyumbani kwa Mkurya wa kawaida vilikuwa vya vigae, miti na vibuyu yaani ebitupa, ebisencho na ebinyongo kwa hiyo chombo cha plastiki kilionekana kama lulu. |
195 |
Kwa hiyo, walioungana na Tanganyika si Wazanzibari bali ni Waunguja. Katika siku za awali, vyeo karibu vyote vilishikwa na Waunguja, na wakati huo kule Pemba mashamba ya karafuu yakaanza kudorora kwa vile wenye mashamba Waarabu walioishi Unguja, walikuwa wamekimbia nchi au wameuawa katika mapinduzi. |
196 |
Haya sasa mashushushu, watawala na raia mmeupata ukweli kafanyeni hima kurekebisha mambo kama mnautaka muungano udumu. Lakini mhakikishe kwanza Wazanzibari na Watanganyika wanapata haki ya kutoa maoni yao na kupiga kura ya maamuzi kama wawe na muungano au la, wasiburuzwe. |
197 |
Imewasilisha bajeti yake Baraza la Wawakilishi. Sawa, hili ni moja ya mahitaji muhimu ya kikatiba ambayo serikali inatakiwa kuyatekeleza. Tatizo ni kwamba akili za wananchi hazipo kabisa huko. Kwa kiwango kikubwa, wananchi wanaotakiwa kufuatilia mjadala wa bajeti mpya, akili zao zipo kwengine. |
198 |
Kila ninavyopima, nabaini kwa kipindi chote hiki, wamezielekeza kwenye Muungano na ndio suala linalowasumbua zaidi kwa sasa. Wazanzibari wanataka kujua hatima ya nchi yao. Wanataka kujua kwani wakitoa maoni itakapokuja Tume ya Mabadiliko ya Katiba, watanufaika kwa lipi. |
199 |
Dola inapozua tafrani kwa makusudi, wananchi wataamua kujihami, wakivamiwa watajitetea, wakijitetea wataumizwa maana hawana silaha isipokuwa mawe na nguvu za miili. Kushindana na askari wenye bunduki si jambo rahisi na matokeo yake mara nyingi ni raia kuumia na kuumizwa. |
200 |
Wanajiuliza vyereje leo nchi ambayo watu wake haijatokea hata mara kupigana kwa sababu ya tofauti ya dini zao, warukiane, kuvamiana na kuchomeana makanisa? Isitoshe, wanasikitika hata msikiti uliomaliza kujengwa upya juzi tu, wa mtaa wa Nyerere, nao umepigwa bomu na polisi. |
201 |
Haiyumkini, wanasema, Wazanzibari ambao ni mchanganyiko wa Wakristo na Waislamu wahasimiane ilhali wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani kwa karne nyingi. Wanawaza lazima kumeingia kidudumtu. Naam. Katika historia ya karne kwa karne Zanzibar, hakujawahi kudhihirika hasama kati ya Waislamu na Wakristo. |
202 |
Taarifa nyingine toka nchini humo zinasema kuwa, ingawa bado muda wa kampeni haujafika rasmi, baadhi ya wanasiasa wameanza kupiga kampeni, jambo ambalo linaonekana litasababisha uchaguzi huo kuwa moja kati ya chaguzi za hatari na zenye vurugu ambazo Kenya haijawahi kushuhudia katika historia yake. |
203 |
Kwa matokeo ya mechi hizi mbili, Taifa Stars inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu na mabao mawili nyuma ya vinara Ivory Coast wenye pointi nne na mabao manne huku Moroco yenye pointi mbili na mabao matatu inashika nafasi ya tatu na Gambia ya nne ikiwa na pointi moja. |
204 |
Anasema majambazi wenye silaha, wakiwa katika boti za kasi, husimamisha boti na mitumbwi ya abiria; kuwatishia, kuwapora na kisha kutokomea kwa kasi. Hata hivyo, matukio hayo ya ukatili kwa abiria wanaosafiri kwa boti na mitumbwi hayaonekani katika taarifa zozote za jeshi la polisi. |
205 |
Watu ni wengi Kibirizi. Kuna vijana wanaopakua mifuko ya chumvi kutoka kwenye malori na kuingiza kwenye boti; na kuna abiria wanaoabiri boti tayari kwa safari. Kuna wavuvi, wajasiriamali na madalali. Kitu kimoja unachoweza kuona haraka ni kwamba makuli na abiria wamelowa maji. |
206 |
Ukoesfu wa umeme wa uhakika nchini ni tatizo sugu. Yamekuwepo mapendekezo mbalimbali ya kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na matumizi ya gesi, umeme unaotokana na nguvu za maji, jua, upepo, mkaa wa mawe, joto ardhi na hata kujenga vinu vya nyuklia kama inavyofanya Namibia na Misri. |
207 |
Dawa zinaharibika kwa kukosa umeme katika maduka ya dawa. Nani atakubali hasara ya kutupa madawa yake? Hii ndiyo sababu ukifanyika ukaguzi hupatikana dawa zilizoharibika zikiwa zinauzwa. Wakubwa wabaona suluhisho ni kununuliwa kwa mitambo inayotumia mafuta ili kuzalisha umeme. |
208 |
Tanzania haipaswi kuwa gizani. Ni uzembe tu na ufisadi unaozunguka sekta ya umeme. Watawala wanunue mitambo ya gesi kwa pesa kutoka ndani ya nchi badala ya kukopa. Tanzania ina makaa ya mawe ambayo hutumika sana duniani kuzalisha umeme. Marekani, China zinategemea makaa ya mawe. |
209 |
Hivyo basi mgodi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma usaidie taifa kuondokana na dhiki ya nishati ya umeme. Mbali ya makaa yam awe, upepo uko kila mahali. Uwezo wa kuwekeza katika upepo tunao, raslimali za kuwekeza katika umeme wa jua zipo. Madini ya ulanga yamejaa tele Morogoro. |
210 |
Usalama wa nishati ya kuni na mkaa uko katika uhakika wa upatikanaji miti. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotumia kuni nja mkaa, uharibifu wa mazingira na misitu yetu umeongezeka hali ambayo inanipa shaka kubwa huko tuendako kwamba si kwema kama hatutafuta ufumbuzi sasa. |
211 |
Hapo kutakuwa na ajira rasmi nyingi kwa vijana wetu. Pili ni kuanza kuhamasisha watu waishio mijini kujenga tabia ya kutumia umeme na gesi kupikia lakini serikali ihakikishe kuwa nishati ya umeme na gesi inapatikana kwa gharama nafuu. Hapo kuna ajira rasmi kwa vijana wetu wanaohitimu ufundi. |
212 |
Tatu ni kufanya mkakati wa kuanza kuzalisha mkaa utokanao na pumba za mpunga. Wachina wanayo teknolojia hii ambayo imewasidia sana katika kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. Tunaweza kujifunza kutoka kwao. Sijawasikia watawala wakilijadili suala la usalama wa nishati ya kuni na mkaa. |
213 |
Wanatuhumiwa kutumia vibaya fedha za umma na sasa Rais Macky Sall amepania kuwafikisha mahakamani. Rais Sall ameapa kwamba atafanya ukaguzi wa wazi ili katika wizara husika na wala msimamo hautabadilika eti kwa sababu mtangulizi wake amerusha shutuma nyingi juu ya kusudio la ukaguzi huo wa wazi. |
214 |
Hakuna kitu kingine kinachoifanya Tanzania kutopata fursa hiyo, isipokuwa ni mfumo duni wa kukuza soka nchini huku nadharia ikitawala vitendo. Programu za kukuza soka zilizopo hazitekelezwi ipasavyo. Tofauti na nchi nyingine, mchezo wa soka Tanzania unachukuliwa kimchezo kama lilivyo jina lake. |
215 |
Kwingineko walikopiga hatua soka ni ajira, tena inayowawezesha vijana wengi kupata maendeleo ya hali ya juu. Siku za nyuma ingawa haukuwepo mkakati wa maana wa kukuza soka nchini, kupitia shule na vyuo wanamichezo wengi hasa wa soka walipatikana na kulisaidia taifa katika michuano mbalimbali. |
216 |
Nchi karibu zote za Afrika Magharibi nazo zinapiga hatua katika soka kutokana na uanzishwaji wa shule za soka za kutosha ambazo zinafanya kazi ipasavyo na kuna vijana wa uhakika wa kujifunza soka na pia kujiunga na klabu za Ulaya kwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa. |
217 |
Mashabiki wanatakiwa kuwa na ufahamu huu wa soka nchini ndipo wapate nafasi ya kulaumu matokeo ya timu uwanjani kulingana na timu pinzani. Hawapaswi kutoa lawama zisizo na kichwa wala miguu kwa matokeo ya aina yoyote ile mbele ya timu zenye mifumo mizuri ya kukuza soka. |
218 |
Madaktari wa aina hii, ndio mwaka jana walisababisha mamia kwa mamia ya watu kutorosha wagonjwa wao hospitalini na kukomba vibubu vyao ili kuwapeleka wapendwa wao Loliondo kwa mchungaji aliyegeuka mganga wa kienyeji. Wakafia huko au wakafa baadaye kutokana na kutekeleza dawa. |
219 |
Inadaiwa pia ndugu wakianza kusutana, kulumbana, kulalamika mbona mnaniachia mgonjwa peke yangu au hata kudai ndugu wengine hawampendi mgonjwa eti huwa nuksi. Wote mnauguza kwanini muanze kudai eti yule yuko vile, ooh mgonjwa akifa sijui mjomba atakuwa umesababisha? Ni dalili mbaya. |
220 |
Kweli, hasira zilizowajaa viongozi wa serikali na vyombo vyao, zimezaa hasara. Sasa nchi, iliyokuwa imetulia kabisa, watu wakienda na kurudi kwenye shughuli za kutafuta maisha, imerudi kwenye hofu kubwa. Rais hakuongoza vizuri au walioelekezwa kuongoza hawakutenda vizuri. |
221 |
Sheikh Mussa alimfuata kijana ambaye akiifuata gari. Alipofika akiwa nje ya gari, huku mlango wa nyuma ya dereva ukiwa wazi, Sheikh Mussa alisalimiana na mtu aliyekuwa ndani. Lakini, ghafla akavutwa ndani ya gari, mlango ukafungwa kwa nguvu, na dereva akaondoa gari kwa kasi. |
222 |
Hakukuwa na kiongozi wa polisi kuthibitisha. Taarifa zilivuja kutoka ndani ya kituo kwamba Sheikh Mussa kweli anashikiliwa pale kituoni. Jitihada za viongozi wa msikiti kusihi Polisi wamuachie na kama kuna tuhuma apewe dhamana, hasa kwa kuwa familia yake haijui, zilishindikana. |
223 |
Taarifa za kukamatwa kwake zikaanza kuenea taratibu mjini. Haikuchukua muda, makundi ya watu wakakimbilia Madema kutaka kujua hatima ya Sheikh Mussa. Kwa kuwa Polisi hawakutaka kujadiliana, walijiandaa kulinda kituo chao na kulinda "mtuhumiwa" wao. Mwanzo wa matatizo ukawa umewadia. |
224 |
Huku watu waliokuwa wanajazana kituoni wakitaka kujua hatima ya kiongozi huyo. Ilipotimu saa 3 usiku, eneo la Michenzani, mita chache kufika Madema likawa limejaa watu wanaofuatilia hatima ya Sheikh Mussa. Ndipo polisi walipoanza kulinda hadhi yao baada ya kuamini wanachezewa. |
225 |
Kwenye saa 5 usiku, eneo hilo likawa limeenea harufu ya kemikali na moshi mzito. Sasa hata waliokuwa wapita njia na waliolala wakalewa sumu. Nilishindwa kupita kwa gari Kariakoo. Palikuwa na kundi kubwa la vijana; barabara imezibwa kwa mawe na mapande makubwa ya zege huku matairi yakiwaka moto. |
226 |
Niliposogea kwa kutembea nikijaribu kufika Michenzani, niliishia kwenye mkunazi, mita 100 hivi kufika. Nikaona magari ya polisi waliosheheni silaha mbele ya ofisi kuu za Idara ya Majenzi. Kila baada ya muda fulani, nikasikia milio ya risasi na mabomu ya machozi zikielekezwa walipo vijana Kariakoo. |
227 |
Tukitaka kwenda mbele tuache unafiki. Tuelezane ukweli hata kama watasema mwandishi au gazeti limenunuliwa na mafisadi kwa maana kama kununuliwa au hapana Mwenyezi Mungu anajua. Wanafiki ni hatari kuliko nyoka. Hata hivyo, nakubaliana na Sitta kuwa taifa linakabiliwa na viongozi wenye sura mbili. |
228 |
Sura ya kwanza ni viongozi mafisadi halisi ambao wako radhi kujiuza kwa vyeo vya duniani hata kama wanajua kuwa kwa kufanya hivyo kutawaumiza wananchi na hasa maskini. Hawa wako radhi kutumia mamilioni ya fedha za walipa kodi maskini kujenga Jumba la Spika kwao hata kama Spika anatoka Njombe. |
229 |
Tuna mifano hai ya viongozi aina hii hapa kwetu. Kwa kuinyonga kihuni hoja ya Richmond bungeni, wakawa wamewasukumiza wananchi kwa Dowans. Dowans walipotaka kujilipa, viongozi haohao kwa unafiki wao wakawataka wananchi waandamane kupinga malipo. Kama walipaji ndio walipwaji, Dowans watalipwa tu. |
230 |
Kutegesha ni kuejenga nyumba au kuwekeza mali katika eneo ambalo halijapimwa ili litakapopimwa na wataalamu fidia iwe kubwa. Sita, mkuu wa wilaya analalamikiwa kwa kitendo chake cha kumwondoa madarakani mwenyekiti wa kijiji cha Nyakunguru, Abeil Maginga kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za kijiji. |
231 |
Mr Treekiller alipofungua kesi mahakamani juu ya hoja hiyo akashinda, jamaa walikata rufaa kupinga. Sasa, baada ya kugundua inaweza kusaidia kupunguza ari, nguvu na kazi ya wenzao kuikimbia bustani ya Eden wakiogopa nyoka, ghafla wamepanga hila nyingine kama za Mabaniani. |
232 |
Lakini kama mtu akiulizwa matunda ya utumishi wake analia kuhujumiwa. Kilio hicho ni kielelezo cha mtu ambaye siku nyingi alikwisha kusahau kuwa cheo ni dhamana, uongozi ni kujitoa, ni kuonyesha mfano ni kukosa usingizi kutokana na kuzongwa na kazi za kutafuta mjawabu ya shida wananchi. |
233 |
Rais anayebaki nchini akajishughulisha na shughuli wanazofanya wananchi, anajijenga. Kwa namna nyingine, inamkurubisha sana na watu wa kawaida. Basi atapendwa hata kama utendaji serikalini si mzuri hivyo. Ni foramu kama hizi humpatia kiongozi hupata hili na lile yanayopita serikalini. |
234 |
Kwenye chakula, vingi vinavyoingizwa kutoka nje, ukiwemo mchele, chakula kikuu kwa Zanzibar, ni vibovu. Mdudu ufisadi serikalini anazidi kustawi na watendaji wanazidi ulafi; huku mazingira yakizidi kuchafuliwa na wakata misitu na wachimba mchanga kwenye fukwe na mabondeni. |
235 |
Wahalifu wanalalamika. Wapishi wanalalamika. Hata walaji wanalalamika. Tumekuwa taifa la walalamishi. Hakuna anayeelekea kujua nini kifanyike ili kukomesha ulalamishi huu sugu unaolikabili taifa. Hii ni dalili ya taifa kukwama katika tope zito ambalo linakwamisha hata wakwamuaji. |
236 |
Kukwama kwa taifa ni matokeo ya kundi linaloitwa mtandao. Kundi hili lilijipanga kuchukua madaraka ya taifa kwa miaka mingi. Likajipenyeza kila sekta. Likafanya kampeni chafu na safi kuhakikisha linachukua madaraka. Watanzania kwa wema wao, wakaliamini na kumchagua Jakaya Kikwete kuwa rais wao. |
237 |
Watu wachache sana watakiri hadharani kuwa wanaridhika na hali ya nchi ilivyo kwa sasa. Kundi hili nalo, licha ya kukorofishana na kusambaratika kila mtu akichukua njia yake, linakiri wazi kuwa wamewaangusha wananchi waliowaamini sana na kuwapa madaraka ya kuongoza nchi. |
238 |
Kwanza, ndilo liliasisi utamaduni wa kuchafuana kama njia ya kujipatia madaraka. Lilifukua makaburi na matundu ya vyoo ili kuanika uozo wa washindani wao. Lilipoona hiyo haitoshi, lilitumia fedha kununua uongozi. Watu walihonga fedha hata wake zao, ndugu zao ili wawapigie kura. |
239 |
Hata Rais Kikwete aliwahi kukiri mara mbili, bungeni na mbele ya vyombo vya habari, kuwa imefikia hatua watu hawaaminiani kiasi cha kutoachiana glasi za maji mezani. Tumeona vituko vingi tangu wakati huo; tangu tuhuma za unga wa kishirikina ndani ya jengo la Bunge mpaka kulishana sumu kwenye taulo. |
240 |
Kauli mbiu ya "siasa ni mchezo mchafu" imepata ushahidi wa kutosha katikati harakati za wanamtandao. Mshikamano wa kitaifa haukuachwa na wana mtandao. Umesambaratika. Wakati kundi hili linaingia madarakani lilikuta taifa likiwa moja hata kama mijadala yenye kuashiria moto wa chini chini ilikuwapo. |
241 |
Risasi ni adui wa amani hata kama inatumiwa na vikosi vya kulinda amani. Hivi sasa hakuna amani katika taifa. Vitendo vya kujichukulia sheria mkononi ndivyo vimechukua nafasi ya mahakama zetu. Benki zimeporwa, vituo vya polisi kuchomwa moto na ofisi za wakuu wa wilaya kuchomwa moto. |
242 |
Kwa mujibu wa Makinda, wateule hao wakishaapishwa kuwa mawaziri, wana haki ya kuanza kufanya kazi za kiwaziri kwenye wizara walizopangiwa. Hata hivyo, Makinda amesema kanuni za bunge zitakuwa zinawafunga wateule hao wa rais kuingia bungeni na kujibu maswali bila kuapishwa kuwa wabunge. |
243 |
Hata mimi sikutarajia kwani katika waandishi sita bora nchini wanaofaa kuteuliwa wakuu wa wilaya mimi simo! Yaani siku ile baada ya kupata orodha ya wakuu wapya wa wilaya, niliisoma orodha ile hadi mwisho, nikarudia mara saba lakini sikuamini kama kweli Mheshimiwa sana kaniacha. |
244 |
Hili litasaidia kukuza ubunifu, uzoefu, utafiti na teknolojia nchini katika nyanja zote za viwanda vinavyogusa reli. Juu ya hayo reli ni usafiri wa uhakika wenye uwezo wa kusafirisha abira wengi zaidi ya mabasi na kwa usalama zaidi. Nini kifanyike? Mosi, serikali imiliki shirika la reli. |
245 |
Kwa mfano treni iendayo kwa kasi ikitoka Mwanza isimame Shinyanga lakini hapo katikati iwepo treni ya kuhudumia vituo vidogo vidogo kati ya Mwanza na Shinyanga. Sita, mfumo wa mawasiliano katika treni uboreshwe ili kuepusha ajali na hasa wakati njia moja tu inatumika kabla ya kujenga njia ya pili. |
246 |
Tisa, tuna nchi sita jirani zinategemea bandari zetu. Reli ingeweza kuzihudumia nchi hizi kwa faida kubwa. Hivyo basi bandari ya nchi kavu kama Isaka ziingekuwa vituo kikubwa vya ajira na biashara. Je, tunashindwa kuyafanya haya? Naamini kwa nia safi na uzalendo tunaweza. |
247 |
Labda tujiulize, kasoro za uteuzi wa wakuu wa wilaya zinazopigiwa kelele na watu wengi zina uhalisia gani? Kwanza, uteuzi umechukua muda mrefu mpaka wilaya zikazoea kutokuwa na wakuu wa wilaya. Kuwepo kwao na kutokuwepo vina uzito sawa. Kasoro hii isifanyiwe mzaha hata kidogo. |
248 |
Pili, kuna madai kuwa Rais Jakaya Kikwete kateua watu asiowafahamu kupitia wasaidizi wake; na kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameishia kutangaza orodha tu. Kimfumo, wakuu wa wilaya wanafanya kazi chini ya wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa iliyo chini ya waziri mkuu. |
249 |
Lakini yeye anaishia kutangaza, siyo kuteua. Kwa upande mwingine pia, wakuu wa mikoa watafanya kazi ya kuwaapisha ma-DC; lakini nao hawakushiriki kuwateua. Aliyeteua mwingine, aliyetangaza mwingine; na aliyeapisha ni mwingine. Utadhani tuna mataifa matatu ndani ya taifa moja. |
250 |
Utata wa uteuzi wa wakuu wa wilaya unakuzwa pia na kazi zao huko wilayani. Mpaka sasa, hakuna mtaalam yeyote wa utawala katika taifa letu ambaye ameweza kuandika au kutamka hadharani, ni nini hasa kazi ya mkuu wa wilaya. Enzi ya Mwalimu, kazi zao zilijulikana na hata kufundishwa darasani. |
251 |
Kazi nyingine zisizo rasmi ni kukisaidia chama tawala kuweka mikakati ya ushindi katika chaguzi mbalimbali. Mikakati yaweza kuwa ya ushindi wa kweli au ya hila. Majukumu mengine kwenye ngazi ya wilaya yana watendaji wake na kwa hiyo kumfanya mkuu wa wilaya agombanie kazi na watendaji wengine. |
252 |
Wakati mkurugenzi na watu wake wanafanya shughuli hizi kwa utaalam, upande wa siasa wa kazi zao unafanywa na madiwani. Mpaka hapa mkuu wa wilaya anakuwa hana kazi. Shughuli za ulinzi na usalama zinasimamiwa vema na afisa usalama wa taifa katika wilaya na kamanda wa polisi wa wilaya. |
253 |
Kwa kuwa majukumu haya yote tayari yana watu, wakuu wa wilaya wanajikuta hawana kazi zaidi ya kushinda wanazunguka na kujitambulisha kuwa wao ndio wawakilishi wa rais katika wilaya. Nafasi hii imepitwa na wakati na hata ikifutwa hakuna atakayeumia kiuchumi, isipokuwa wanaoitafuta kwa udi na uvumba. |
254 |
Dk. Shein huna haja ya kukasirikia wananchi. Badala yake ni muhimu sana utambue kuwa hata wao wanaipenda nchi yao kama uipendavyo wewe na ujivuniavyo kuiongoza. Wanaipenda sana. Hebu afikirie kwani wananchi wanaposema "hatutaki Muungano huu" unadhani tafsiri ni kutaka uvunjike au uvunjwe? Hapana. |
255 |
Sasa si ndivyo waonavyo? Kumbe mtu kufikiri hivi anakusumbua rais? Dk. Shein kama unataka kuongoza vizuri, basi zingatia vilio vya wananchi unaowaongoza. Tena ungeshukuru na kufurahia kuwasikia wanasema au kulalamika hadharani. Kama hujanielewa ninachokusudia, panda ndege hadi London. |
256 |
Kumbuka tayari Wazanzibari kiasili ni watu wenye akili sana, wanafikiri kabla ya kuamua, wanauliza maswali wakitaka majibu. Dk. Shein unajua vizuri kwamba kwa sababu ya ukweli huo, ndio maana Wazanzibari wengi wanafanya kazi kubwakubwa kwingineko Afrika, na hasahasa Marekani, Ulaya na Uarabuni. |
257 |
Ukitambua hili huwezi kupata shida kuwaongoza. Utakuwa unajua tangu awali unao watu makini ambao ukiwatumia vizuri watakusaidia kuibadilisha nchi iwe kweli ya maziwa na asali badala ya tope na harufu mbaya. Ila ukiamua kuwapuuza na kuwakandamiza, utabaki kuongoza kwa shida. |
258 |
Hili liwe fundisho kwa wakuu wa wilaya wote na wenzao wakuu wa mikoa ambao wanatanguliza maslahi ya chama chao badala ya maslahi ya Wananchi na Taifa kwa ujumla. Wakuu wa wilaya, kama walivyo wakuu wa mikoa, ni makada wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanawekwa kwenye wilaya au mikoa kumwakilisha Rais. |
259 |
Kutokana na kosa hilo, hawawezi kushiriki katika vikao vya bunge hadi watakapoapa kiapo cha uaminifu wa Bunge. Lakini mwanasheria mkuu wa serikali anayepaswa kuwa mjuzi wa sheria na katiba, Frederick Werema anasema hao ni wabunge. Rais wa wanasheria wa Tanganyika anasema katiba iko kimya. |
260 |
Mabadiliko ya watu peke yake hayana maana yoyote. Bila kwanza kuweka msimamizi madhubuti kinachofanyika ni kubadilisha walaji tu. Kama lengo ni kumshirikisha kila mkuu wa wilaya, mkoa, au mawaziri na wengine nchi itabaki mifupa mitupu katika hii miaka mitatu ya mashaka iliyobaki. |
261 |
Kwamba mkuu wa wilaya ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, lakini pia ndiye mwakilishi wa rais katika wilaya. Kwa maneno mengine mkuu wa wilaya ni halali wilayani kwa sababu tu anaiwakilisha serikali kuu ngazi ya wilaya. Nilimkubalia kwa hoja zake. |
262 |
Sina sababu ya kukataa hoja ambayo imekwisha kuanza kupigiwa chapuo kwamba kuendelea kuwa na nafasi za wakuu wa wilaya kwa mfumo wa sasa na kutaka pia kuwa na halmashauri zenye nguvu na zinazowajibika, ni sawa na kuwa na mifumo miwili sambamba ya utawala, yote ikiendeshwa kwa kodi za wananchi. |
263 |
Mwanawasa alifariki katika kipindi cha pili cha uongozi wake kutokana na ugonjwa wa ghafla wa mapigo ya moyo, naye Mutharika alifariki katika kipindi cha pili cha uongozi wake kwa ugonjwa kama uliomuua Mutharika. Vifo vyote viwili vilitabiriwa na nabii maarufu wa Nigeria, TB Joshua. |
264 |
Wenger anasifiwa na kutolewa mfano hata na Fifa kwa kusajili vijana wasio na majina kuwanoa hadi wanakuwa hatari kisha huwauza kwa bei mbaya. Kila linapotokea shinikizo la mashabiki aondoke, wamiliki wa klabu hiyo wamekuwa wakizingatia faida ya kifedha na siyo faida ya kisoka. |
265 |
Lakini viongozi wa Simba wanajua vizuri ghadhabu ya wanachama. Wanachama waliwahi kuvamia nyumbani kwa aliyekuwa mwenyekiti wao Juma Salum wakafanya fujo na wakachoma uzio. Kiongozi wa hivi karibuni anayeweza kueleza adha ya wanachama katika klabu hiyo ya Msimbazi ni Hassan Dalali. |
266 |
Lakini pia, kauli hii ya Kandoro inatoa ujumbe mahususi kwa umma, kwamba uteuzi wa Rais Kikwete unavuja mapema na kuwafikia wananchi kabla ya muda wake. Cha ajabu zaidi, ni pale Kandoro anaposema Kimolo amepewa barua ikimweleza kuwa hatakuwamo kwenye orodha ya wakuu wa wilaya. |
267 |
Nikiamini kwamba Kandoro ameteleza na kudandia shughuli ambayo si yake, bado natega masikio kusikia kauli ya Rais Kikwete juu ya uamuzi wa DC Kimoro na sababu zake za kujiuzulu, huku nikilinganisha na sababu alizoeleza Kandoro akitaka umma uziamini bila kujali kwamba zinaidhalilisha serikali. |
268 |
Pale mwenzako asipofahamu lugha unayoitumia, muhimu utafute lugha atakayoifahamu. Kubadilisha Katiba imekuwa lugha muwafaka kuwafanya wenzetu waone nini tunataka. Marekebisho ya Katiba yameibua lawama tele kutoka kwa wanasiasa na hata miongoni mwa wanasheria mahiri Bara. |
269 |
Si ingetosha tu kuuliza Watanzania kama wanautaka au hawautaki? Kungekuwa na haja gani ya kutaka uwe madhubuti kama wengi hawautaki? Wazanzibari wakisema hawautaki, dawa iliyobaki ni moja tu: kumaliza taratibu mambo ya muungano. Udugu wa watu wetu na mahusiano ya kidiplomasia vitandelea. |
270 |
Kila mmoja anafahamu fika kwamba kiini cha umaskini wetu si uvivu wa wananchi kama wenye dhamana wanavyosema, bali kiini ni watawala na watendaji walafi, wabadhirifu na mabingwa wa ufisadi. Watawala hawa wanadhulumu na kunyonya haki za watu kwa mori kubwa, motisha kubwa na msukumo kubwa. |
271 |
Hawana huruma kwa wajane wanaohangaika kila siku kutafuta riziki za kuwalisha yatima. Hawana huruma kwa yatima wenye vipaji wanaokosa fursa ya kwenda shule kwa sababu mama hana pesa ya mchango wa dawati. Hawana huruma kwa wajawazito wanaojifungulia sakafuni katika hospitali zetu. |
272 |
Uchumi gani huo unaokua bila kukua mifukoni mwa watu? Maana ya kukua kwa uchumi ni kuinuka kwa hali ya maisha ya watu. Ni uchumi upi mnauongelea? Labda uchumi wa mafisadi maana huo unakua kwa kasi zaidi. Tuhabarisheni. Wananchi wanapewa ahadi hewa za kinafiki. Mnafiki akitoa ahadi hatimizi. |
273 |
Ukiuangalia uzembe unaofanywa mfano katika suala la umeme, msongamano wa magari ya Dar es Salaam, kulegalega kwa usafirishaji wa reli, kufa kwa shirika la ndege, viwanda vyetu kutokuzalisha, mikataba mibovu ya madini na uwekezaji, utakubaliana nami kwamba Tanzania haipaswi kuwa ombaomba. |
274 |
Bila nia ya kizalendo huwezi kuondoa umaskini kwa kuendelea kukumbatia ufisadi na uozo. Bila nia yenye huruma huwezi kuondoa umaskini kwa ajira za uchuuzi. Bila nia thabiti huwezi kuondoa umaskini pasipo kutengeneza ajira zenye mafao ya uzeeni. Yote haya yanategemea nia njema ambayo haipo. |
275 |
Wakati umefika sasa tutambue kwamba kuendelea kukua kwa umaskini na kukua kwa ufisadi kunahatarisha amani ya nchi yetu. Niliwahi kusema hapa kuwa jeshi la vijana wasio na ajira ni kubwa na huwezi kulidhibiti kwa bunduki, risasi na mabomu bali kwa ajira, huduma, matumaini ya maisha bora. |
276 |
Watakachosema, ndicho tutakachonukuu na hatimaye kuwasilisha, ameeleza mjumbe kutoka Zanzibar. Mjumbe kutoka Bara alipoulizwa iwapo misimamo yao kuhusu Muungano itazuia kukusanya maoni ya wananchi yanayopingana nao, alisema suala la kuujadili Muungano haliwezi kuzuilika. |
277 |
Ndani ya nafsi zao wanajua kuwa misimamo yao hiyo ya kujitia kulinda muungano kimabavu, inatofautiana na maoni ya wananchi. Sasa unapokuta msimamo wa wananchi katika jambo hili unatofautiana na ule wa viongozi wao, ujue tunalo tatizo. Lakini, katika hali hii, aghlabu, wenye tatizo huwa ni viongozi. |
278 |
Safari imesimama na kazi ya kuokoa imekuwa ikiendelea kitambo sasa. Baadhi ya abiria waliobahatika kuopolewa, wameonyesha tabia ya ajabu pale wanapojirusha tena majini na kufanya kazi ya uokoaji iwe ngumu zaidi. Sinema hii inaendelea na haionyeshi kuwa itakuwa na mwisho mzuri. |
279 |
Hili halikufanyika na litamgharimu sana rais pamoja na chama chake. Kosa la kwanza la kukosekana kwa mchakato makini limekwishaonekana. Hili linahusu rais kuteua wabunge na halafu kuwateua kuwa mawaziri na hatimaye kutangaza kuwaapisha kuwa mawaziri kabla ya kuapa kuwa wabunge. |
280 |
Anaweza kuahirisha kuwaapisha kuwa mawaziri mpaka bunge likae, lakini tayari kosa kubwa limefanyika na kutia dosari mchakato mzima wa uteuzi na uendeshaji serikali. Katika serikali makini, dosari hii ingeondoka na mtu huko ikulu; lakini kwa kuwa kuna ombwe la uongozi, hilo haliwezi kutokea. |
281 |
Kwanza, serikali hii inakabiliwa na tatizo kubwa la utawala bora. Mambo ya kiserikali, siri na taratibu zake, yanaenda ovyo. Ni mwenendo huu ambao umefanya Mkuchika kuteuliwa kuwa waziri wa wizara inayohusika na idara nyeti kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Usalama wa taifa. |
282 |
Bila kujali tofauti zao binafsi tusizojua chanzo chake, tukubaliane kimsingi kuwa kilimo na maji ni vitu viwili muhimu. Aliyeshindwa Kilimo hawezi kuongoza Maji. Ukiacha Mkuchika na Maghembe, hawa wawili ambao wamepigiwa kelele karibu na kila mtu, kikosi kizima hakina muunganiko. |
283 |
Kwa naibu mawaziri, huko ni vurugu tupu. Baada ya kufichuka siri za jinsi wanavyovurugana na mawaziri wao, kuongeza idadi yao siyo tija, bali ni kuongeza gharama. Mpaka sasa, hakuna kazi maalum ya naibu waziri inayojulikana, zaidi ya kujibu maswali yaliyoandikwa bungeni. |
284 |
Hivyo basi tunapaswa kujiuliza kwa nini hakuna ajira, kwa nini ubora wa elimu umeshuka sana, kwa nini huduma ni za ovyo katika hospitali na ni namna gani mifumo yetu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii inarekebishwa katika nchi. Hiki ndicho kiini ambacho hakiguswi na dawa kutoka Benki ya Dunia. |
285 |
Na juu ya hayo mfadhili anapokata pesa basi hospitali nayo inazikwa. Unaweza kutengeneza ajira nyingi tu za wachuuzi na machinga kwa kuwapa mikopo ambayo ina riba kubwa. Matokeo yake wanaishia kufanyia tumbo tu na benki. Hakuna faida. Hawawezi kujiwekea akiba kwa kuuza vitana na leso. |
286 |
Hili ndiyo suluhiso sahihi lililokuwa ndani ya Azimio la Arusha. Mtazamo wa pili ni ule wa nchi tajiri za magharibi kuziwezesha nchi maskini katika nyanja za menejimenti na usimamizi wa biashara, kilimo, uchimbaji madini, uvuvi, ufugaji kupitia uwekezaji ili kuongeza uzalishaji. |
287 |
Pia kutoa msaada wa kitaalamu wa kuwasaidia watu katika nchi maskini kuongeza uzalishaji katika kilimo na mifugo na namna ya kupata mikopo kwa wanaojiajiri katika sekta isiyo rasmi, na kuwapa mafunzo ya kuboresha uzalishaji wao. Lakini katika uhalisia wa mambo wawekezaji hawalipi kodi. |
288 |
Mtiririko wa maswali uliendelea. Kwanini hakuna mtindo mmoja wa kuandika maelezo ya picha? Kwa nini picha zinawekwa katikati ya ukurasa, karibu kwa kurasa zote za ndani? Kwa nini picha hii imeiva sana kuliko nyingine? Walijibwa. Ni kukosoa. Ni kutaka majibu kwa ambacho hakikueleweka. |
289 |
Bali ni kusahihisha gazeti lisilosahihika kwani tayari liko mitaani. Je, huu ni mzaha? Hapana. Hili ni darasa. Kwa magazeti yanayotoka kila siku, basi kila siku kuna mjadala juu ya gazeti lililotoka. Kwa gazeti la kila wiki, basi siku ambapo linatoka, hujadiliwa kwa kina. |
290 |
Lifuatiliwe? Majina yameandikwa kwa usahihi? Shabaha ya darasa hili ni kujadili bidhaa iliyotoka kiwandani na kuanza kuandaa bidhaa nyingine iliyo bora kama hii au yenye ubora zaidi. Hapa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Tumaini walishiriki kikamilifu. Wakati mwingine ukosoaji huwa mdogo. |
291 |
Mimi nadhani wameonewa na kwamba wanapaswa kusikilizwa. Mimi sioni sababu kwa nini kusifanyike kura hiyo ya maoni kwa Watanzania wote, siyo Wazanzibari peke yao, ili kwa pamoja tuamue kama taifa, kama muungano huu tunautaka kweli au tunaburuzwa na wanasiasa ambao wana maslahi wanayopigania. |
292 |
Wakati huo Chama cha Kamahuru cha Pemba kilikuwa kimemaliza kuungana na chama cha James Mapalala wa Tanganyika ili kiweze kuwa halali kutokana na sharti lililowekwa, kwamba ili chama cha siasa kiweze kushiriki siasa za Tanzania lazima kwanza kiweze kuwa na wanachama pande zote mbili za muungano. |
293 |
Sikukubaliana na Jecha wakati ule na mpaka leo sikubaliani na maoni kwamba wananchi kushiriki uchaguzi mkuu au mdogo ni ishara kwamba wanaupenda muungano. Ninaamini kuwa unafiki huu wa wakubwa kuupenda muungano wakiwa madarakani na kuuchukia wakitoka utamalizwa na kura hii ya maoni. |
294 |
Kama wananchi wanautaka muungano basi Tume ya Warioba iende mbele na kuanza mchakato wa kukusanya maoni ya katiba ya nchi na kama wasioutaka muungano watakuwa wengi basi moja kwa moja tuanze na mchakato wa maoni ya katiba ya Tanganyika kwa Watanganyika na ya Zanzibar kwa Wazanzibari. |
295 |
Pia wapo Watanganyika wengi wanaoshindwa kuwaelewa Wazanzibari hasa wanapolalamikia kulipishwa ushuru wa forodha bandarini Dar es Salaam, Tanga au Baamoyo wakati wanafahamu fika kwamba kule Zanzibar wanalipishwa ushuru kwa viwango vya chini kuliko vinavyolipwa Dar es Salaam. |
296 |
Ugumu wa maisha kwa wananchi hauonekani kwao; wamejikita katika mambo madogomadogo ambayo yana mwonekano wa anasa, usanii na utoto mwingi. Misiba isiyokuwa na tija ndiyo wanaikimbilia kuhani huku nyuma wanatuletea siasa za udaku, fitina na majungu. Miaka inakwenda, moja jema la mfano hakuna. |
297 |
Sijui nani katoa wazo mufilisi kama hili. Ni aibu kwa watu hawa kungoja kuwajibishwa na kuondoshwa kwa aibu badala ya wao wenyewe kuwajibika na kuondoka wakiwa na heshima zao. Wanafanya watu wahisi kuwa walijua kuwa aliyepaswa kuwawajibisha asingewawajibisha kwani ni mwenzao. |
298 |
Mwenyekiti anashangaza maana kama vyama vya siasa vimeazimia kwenda kwa wananchi kukusanya saini zitakazotosha rais mwenyewe kupigiwa kura kutokuwa na imani naye, kutochukulia hoja hii katika umuhimu unaostahili ni bahati mbaya. Tukiuchekea utoto huu tunaikejeli amani yetu. |
299 |
Mawaziri wanateuliwa na rais na kufanya kazi kwa ridhaa yake. Inapotokea watu na vyombo vingine nje ya rais vikawakataa wateule wake, basi anayekataliwa siyo wao, bali ni rais. Mawaziri wanapata shida kukubaliana na shinikizo la kujiuzulu kwa kuwa rais aliyewateua yupo na hajaonyesha kuwachoka. |
300 |
Rais ana akili timamu. Ana vyombo nyeti vinavyompa taarifa juu ya utendaji wa mawaziri. Lakini amekuwa kimya kwa kuwa ameridhika na utendaji wa mawaziri wake. Mawaziri hawa wana ruhusa ya kumwona rais wakati wowote na mahali popote. Wanaongea naye bila kupitia kwa waziri mkuu. |
301 |
Baadhi yao ni marafiki zake binafsi na kikazi; zaidi ya hata waziri mkuu na makamu wa rais. Wanaweza kumwambia rais mambo ya waziri mkuu kuliko hata waziri mkuu anavyoweza kumweleza rais juu ya mambo yao. Inawezekana hilo, ndilo linalomfanya rais kujikuta yuko kitanzini. |
302 |
Inawezekana hali hii imetokana na muundo wa serikali ulivyo, lakini zaidi mgogoro huu unashinikizwa na haiba ya rais aliyepo sasa. Rais wetu yuko tayari kuumia yeye kuliko kuwaumiza marafiki zake. Yuko tayari kuliumiza taifa, bunge, chama chake na hata serikali nzima, kuliko kuwaumiza marafiki zake. |
303 |
Wameangusha kilimo. Nchi inazalisha sukari kwa wingi, lakini inanunua sukari kwa bei ya juu sana kuliko wanaonunua sukari kutoka kwetu. Wakulima wanatumia jembe la mkono, lakini tunaambiwa kuna matrekta yameagizwa kwa ajili ya kilimo. Yameishia bandarini kubeba makontena ya mawaziri. |
304 |
Wanataka wawajibishwe badala ya kujiuzulu. Kwa nini tusifikiri kuwa kuna jambo kubwa wanasubiri kufanya ndipo waondoke kwa utulivu? Mawaziri wameangusha sekta ya nishati kwa kubinafsisha kila kitu na kuweka mikononi mwa wachache na wao kujichukulia tenda na mikataba ya kuendesha nishati ya umeme. |
305 |
Mara wasafirishe mafuta mazito wao wenyewe, mara wasafirishe nguzo za umeme, mara wawe ndio wasambazaji wa mita za umeme na mara wasambaze mafuta ya magari. Mambo ni mengi. Tunaambiwa, na hizi ni taarifa za ndani ya serikali, mawaziri hawa na marafiki zao sasa ni matajiri kuliko shirika la umeme. |
306 |
Kwa nini tusifikiri kuna jambo wanasubiri kulifanya, tena lililokubwa zaidi? Mawaziri hawa wameangusha hospitali zetu na sekta nzima ya afya hapa nchini. Hospitali zote zimekuwa uwanja wa harakati za wafanyakazi kudai haki zao, badala ya kuwa eneo la wagonjwa wanaotafuta tiba. |
307 |
Hakuna maji. Hakuna umeme. Hakuna vifaa vya tiba. Kinachoonekana kuongezeka mahospitalini ni kukosekana kwa utu, huruma na uzalendo. Wagonjwa hawahurumiwi, fedha ya umma haihurumiwi, na nchi haihurumiwi. Lakini bado wakubwa wetu, wakiwamo mawaziri wa wizara hii, wanakwenda ng'ambo kwa matibabu. |
308 |
Huyu akiambiwa ajiuzulu, utasikia anagoma. Hatimaye utasikia rais amembakisha serikalini. Wala rais hajiulizi, iwapo waziri huyu ameweza kusafiri na bunduki za kivita katika gari la serikali, atashindwaje kutumia madaraka yake kujitajirisha? Kuna mambo mawili tunayoweza kutafakari haraka. |
309 |
Tusemeje? Kwamba hata rais amejiunga na kundi baya lenye lengo baya kwa taifa? Pili, hawa mawaziri hawajaridhika na vile walivyoviangusha. Wanasubiri wamwangushe yule aliyewateua ndipo waridhike kuwa wanajua kuangusha. Tukifikia hatua hiyo, Tanzania haitakuwa mahali pema tena. |
310 |
Tayari serikali imemhusisha Henry, mtoto mwingine wa Banda kuhusiana na ushiriki wake katika uuzwaji wa shirika la taifa la simu katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa baba yake. Henry, ambaye kwa sasa yuko Afrika Kusini amesema kwamba hatua hiyo ina msukumo wa kisiasa. |
311 |
Mawaziri hawa wameshutumiwa waziwazi ndani na nje ya bunge. Wachache kati yao wamejitetea na wengine wamekaa kimya. Pengine hii ndiyo sababu Rais Kikwete amevuta subira akiwa safarini Brazil na baadaye Malawi, ili apate fursa ya kuchambua ili kubaini pumba ipi na mchele ni upi. |
312 |
Itakumbukwa hata katika kipindi chake cha kwanza, alilazimika kuunda upya serikali baada ya kujiuzulu waziri wake mkuu wa kwanza, Edward Lowassa na mawaziri wawili wengine kutokana na kashfa ya kushinikiza mkataba wa ukodishaji wa mitambo ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond. |
313 |
Ugumu wa maisha umesababishwa pamoja na sababu nyingine nyingi, ikiwamo ya ufisadi wa kupindukia katika wizara hizo. Wakati tamko la Pinda likisubiriwa kwa hamu sana, zipo tetesi kuwa Rais Jakaya Kikwete amesita kukubaliana na kujiuzulu kwa mawaziri wake hao kwa sababu kadhaa. |
314 |
Alilisema hili baada ya kutangaza kusimamishwa kazi kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Mganga mkuu wa wizara hiyo. Baada ya Rais kurejea nchini, siyo tu kuwa alipuuza ahadi ya Pinda kwa madaktari bali alikataa hata kupokea barua ya kujiuzulu iliyoandikwa na Waziri wa Afya. |
315 |
Hii ilitokana na mjadala wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyohusu mahesabu ya serikali za mitaa, serikali kuu na mashirika ya umma. Mawaziri wahusika waliitwa mafisadi, wezi wakubwa na kwamba walistahili kunyongwa hadharani kwa sababu wanawatesa wananchi wasio na hatia. |
316 |
Wengi wao wakamkubalia na wachache sana wakamgomea. Kitendo cha mawaziri kumgomea Waziri mkuu, kiongozi wao na mkuu wa shughuli za serikali bungeni, kingetosha kumfanya awaweke pembeni ili rais akirudi toka safari awarejeshe kazini au athibitishe hatua ya Pinda kama anamheshimu. |
317 |
Mabwana hawa huwa mabingwa wa kutafuta njia mbadala ya kuahirisha kero au matatizo ya nyumbani. Baadhi huwa chapombe wakidhani wakiamka asubuhi matatizo yatakuwa yameisha. Halafu wengine huamua kujificha nyumba ndogo. Omba usikutane na mwanaume mwenye matatizo na ndoa yake. |
318 |
Baba yetu anashinda misibani bila kujali inamhusu au la mradi tu asikae nasi muda mrefu. Wanamwita Mzee wa Misiba, eti anatamani watu wafe ili apate pa kushinda. Anatia huruma na unaweza udhani siye aliyekuwa anakosa usingizi usiku kucha kwa kumuwaza huyo aliyekuja kuwa mkewe. |
319 |
Akina baba wenye vijisenti, hasa kama ni mabosi kazini, kama baba yetu, wao huwa safarini kila mara; mikoani au nje wakibadili ndege kuhudhuria mikutano hata isiyo na tija. Siku wanapolazimika kufika nyumbani huwa ni kubadili nguo tu. Hakuna mazungumzo ya upendo na familia. |
320 |
Baba anapofika mahali akajali zaidi safari kuliko familia, mke hujuta kuolewa, na watoto hujuta kuzaliwa na baba asiyewathamini. Ukweli sote tunajuta; majuto makubwa kabisa. Kaka yetu anataka kunyang'anywa cheo Mjengoni, baba hajali; na ndugu zetu wanafilisi duka baba hajali. |
321 |
Siku watoto wakiona mama yao anapigwa na baba msafiri hujitosa kuamua. Watoto wanaojua mama yao anaonewa hasa kutokana na anavyohangaika kuwalea humsaidia mama yao kumpiga baba, lakini wasiojali huona mke ni wa kupigwa tu. Huu ndiyo mwanzo wa baba na mama kutoa huduma kwa watoto kwa upendeleo. |
322 |
Je, baba yako anakusikiliza na kukujali? Ukinijibu baba yako anakujali, halali misibani na hasafiri unataka kujiridhisha tu. Yule mjomba mkubwa aliyesomea fedha na kule kazini ni maarufu kwa jina la utani la Sieyijii, amesema baba anawapenda mno mafisadi hata kama wanamtia hasara. |
323 |
Lakini Afrika inazidi kudorora chini ya utawala bora usiothamini haki za watu, usawa wao, utu wao na ustawi wao. Tufahamu kwamba utawala bora hauna maana ya utawala wa sheria zinazolinda haki ya umma. Pili hauna maana kuwa ni uongozi bora unaoendesha serikali kiadilifu. |
324 |
Kisheria Katiba ya Ivory Coast ilimpa ushindi na kuhalalisha utawala wake. Alifanya dhuluma kupitia upenyo wa utawala bora wa sheria. Utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini nao pia ulikuwa utawala bora kisheria kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini zilizotungwa na bunge na kutekelezwa na mahakama. |
325 |
Wabunge walipigiwa kura wapigakura walijiandikisha kisheria. Utawala huu ulitambuliwa kimataifa. Lakini utawala wa makaburu haukuwa wa haki ingawa serikali yake iliundwa kisheria. Utawala bora wa kisheria usiozingatia haki umeigawa Afrika katika matabaka ya mabwana na watwana. |
326 |
Wengine hutumia vyama vya siasa kuwaondoa watawala kama ilivyokuwa kwa Thabo Mbeki Afrika Kusini. Wengine hutumia nguvu ya hoja na kushinda kama Tanzania. La kusikitisha sana watawala hawazisomi alama za nyakati na kujisahihisha na kuwa viongozi. Wanashikilia uzi ule ule. |
327 |
Kama wanajua kuwa hii ndiyo hatima basi kwa nini wanaendeleza utawala wa dhuluma, unyonyaji, mauaji, rushwa na ufisadi? Afrika itaweza kustawi iwapo itajenga mifumo imara wa kisheria na kimaadili inayoheshimu haki, utu na usawa ambayo italeta tumaini, upendo, umoja, amani na ustawi kwa watu wake. |
328 |
Na mwenye kuvunja ahadi ni mnafiki. Wale waliopewa dhamana ya uongozi na wananchi ya kuwawakilisha wanao wajibu mkubwa wa kuhuisha dhana ya uongozi bora ili kurejesha uadilifu na uaminifu katika uongozi ambao utasimamia kwa haki kukua kwa demokrasia, uchumi na maendeleo ya watu wa Afrika. |
329 |
Uamsho wanahamasisha watu watoke na kusema hawapo tayari kuchukuliwa mamlaka ya nchi yao Zanzibar na kwa hivyo hata katiba inayoandaliwa, haiwahusu, bali wanachotaka serikali yao, Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kwanza iitishe kura ya maoni ili wananchi watamke kama wanataka au hawataki muungano. |
330 |
Wanasheria, wakiwemo wale waliojumuika pamoja na kuanzisha asasi iitwayo Baraza la Katiba Zanzibar kwa ajili ya kuhamasisha watu Unguja na Pemba kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ndio hasa wanaojenga hoja ya kwamba sasa ni vema kuwe na muungano wa mkataba. |
331 |
Kumpiga mwamuzi hakubatilishi matokeo ya mchezo na wala hakufuti adhabu aliyoitoa; zaidi wachezaji au viongozi au mashabiki au makocha watajihatarisha kufungiwa tu. Jambo zuri ni kwamba mwamuzi anayebainika kwamba amepokea kishawishi kutoka upande mmoja wa timu hufungiwa. |
332 |
Mwamuzi anaweza ashindwe kumudu mchezo kwa sababu ya hofu ya mechi au anachelewa kutafsiri sheria, hivyo atakuwa hapigi filimbi kwa wakati faulo ikifanyika au anapiga wakati si faulo kubwa kiasi hicho. Kuchelewa kupuliza filimbi kunaweza kuhesabika kuwa anavunja "muv" yaani shambulizi. |
333 |
Aidha, anaweza adhani mpira umepita mstari au haujapita. Kama umepita je, umetoka nje hivyo mpira ni wa kurusha au golikiki au ni bao na kama haujapita mstari, je, siyo bao, siyo kona au haujatoka? Hapa ndipo ulipomjadala sasa wa haja ya kutumia vifaa maalumu ili kuamua. |
Комментарии